Baadhi ya wafanyabiashara wa Vingunguti Machinjioni wakiperuzi Gazeti la Amani kwa pozi.
Na Gabriel Ng’osha/GPL
Wasomaji wa viunga mbalimbali vya jiji la Dar leo wamelisifia Gazeti la Amani kutokana na kuboreshwa kwa habari, simulizi, machombezo na hadithi na habari nzuri za uchunguzi.
Timu ya Promosheni ya Gazeti la Amani ambalo linatoka kila Alhamisi ilizunguka Kinondoni, Buguruni, Vingunguti, Segerea, Tabata na kwingineko ambako wasomaji walio wengi walililisifia gazeti hilo kwa kuboresha.
“Gazeti la Amani ni kweli limeboreshwa naona hadithi nzuri na zakutosha, endeleni kutupa kile kicho bora wasomaji wenu, kwani tunawaamini sana kwenye habari za uchunguzi na mastaa,’’alisema Jeremia Sadick mkazi wa Buguruni, Dar.