JESHI la Polisi Mkoa wa Mwanza linawashikilia watu watano kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya watu watatu katika tukio lililotokea Desemba Mosi, mwaka huu.
Waliouawa ni 1. Dotto Coastantine @ Makanyanga miaka 19, Msukuma, 2. Bakari ambaye hakufahamika jina la pili mwenye umri kati ya miaka 20 hadi 25 na mtu wa tatu hakufahamika jina umri ni kati ya miaka 20 hadi 25.
Marehemu hao wanadaiwa kuwa wakazi wa Nyakabungo B waliuawa kwa kupigwa fimbo na mawe katika sehemu mbalimbali za Miili yao na kundi la watu wanaidaiwa kujichukulia sheria mkononi baada ya kuwatuhumu kujihusisha na vitendo vya wizi na Ubakaji.
Tukio hilo lilitokea tarehe 1.12.2019 majira ya saa 19:45 HRS, huko Mtaa wa Nyakabungo B Wilayani Nyamagana hii ni baada ya vijana hao (Marehemu) kupita mtaa wa Nyakabungo B ndipo walipokunata na watu walioanza kuwakimbiza na baadae Mwenyekiti wa mtaa huo Abdulkadri Yunusu @ Jacobo miaka 55 Mhaya, Alipiga filimbi huku akitamka kuwa watu hao ni wezi na baadae watu waliwakamata na kuwafunga kamba kisha kuwapiga mawe na fimbo hadi wakapoteza maisha.
Watuhumiwa waliokatamatwa kuhusiana na Mauaji hayo ni;
1. Abdulkadri Yunuso @ Jacobo miaka 55 Mhaya mwenyekiti wa mtaa wa Nyakabungo B.
2. Ezekiel Zephania @ Senso miaka 35 Mkurya ambaye aliwafunga Kamba Marehemu .
3. Athuman Chacha miaka 45, Mkurya
4. Ramadhan Athuman miaka 48
5. Hamis Peter Miaka 22 Mkurya wote wanadaiwa kuhusika kuwafunga Kamba marehemu.
Jeshi la Polisi linaendelea na upelelezi wa tukio hilo na uchunguzi ukikamilika watuhumiwa watafikishwa Mahakamani, Aidha ufuatiliaji wa kuwatafuta watu wengine waliohusika kwa namna moja au Nyingine na tukio hilo bado unaendelea. Miili ya Marehemu imehifdhiwa Hospitali ya mkoa wa Mwanza Sekou toure kwaajili ya uchunguzi na Utambuzi.
Kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza anatoa Onyo kwa Mara nyingine Wananchi wenye tabia ya kujichukulia sheria Mkononi waache Tabia hiyo na waviache vyombo vya dola vifanye kazi yake kama mfumo wa utawala wa Sheria unavyotaka, Kufanya kinyume na watuhumiwa walivyofanya ni kosa la jinai na madhara yake ni kushtakiwa Mahakamani.
Imetolewa na
Muliro J. Murilo – ACP
Kamanda wa Polisi Mkoa wa mwanza
Desemba 2, 2019.
Na Johnson James – GPL Mwanza.