The House of Favourite Newspapers

Watu 10 Wapoteza Maisha kwa Shambulizi

0

TAKRIBAN watu 10 wamefariki katika kaunti ya Wajir  nchini Kenya, jana (Ijumaa) baada ya watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa kundi Al-Shabaab kushambulia basi liitwalo Medina. Kati ya waliofariki wapo polisi saba ambapo watu wanne  walijeruhiwa.

 

Watu hao waliokuwa na bunduki walilishambulia basi lililokuwa likielekea Mandera, kati ya Wargadud na Kaunti ya Wajir mnamo saa 11:30 jioni walipolisimamisha na kuwatenganisha abiria katika makundi mawili  na walipoliachilia basi waliwaua watu kumi.

 

Taarifa za serikali zinasema basi hilo lilikuwa na abiria 36 wakati wa tukio hilo.

 

Mkuu wa Kaunti ya Wajiri, Loyford Kibaara, amesema watu wanne walionusurika walitoroka kupitia madirisha ya basi hilo, miongoni mwa ni polisi watatu na raia mmoja.

 

Chanzo: Daily Nation

Leave A Reply