The House of Favourite Newspapers

Watu 12 Wauawa Katika Shambulio Mandera, Kenya

mandera

Takribani watu 12 wanahofiwa kufariki baada ya watu wenye silaha kushambulia eneo moja la malazi mjini Mandera, kaskazini mashariki mwa Kenya.

Maafisa wa polisi wamesema watu 12 wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa huku polisi na wanajeshi wakifanya msako na kushika doria mjini.

Taarifa zinasema milipuko mitano ilisikika kabla ya ufyatulianaji wa risasi kutokea.

Mji wa Mandera umekuwa ukishambuliwa mara kwa mara na wanamgambo wa Al-Shabaab, kundi linalopigana dhidi ya serikali inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa katika taifa jirani la Somalia.

Wanamgambo hao wamekuwa wakishambulia watu ambao si wa asili ya Kisomali.

Comments are closed.