Watu 14 Wauawa kwa Shambulio Kanisani

ZAIDI ya watu 14 wameuwawa baada ya shambulio la kigaidi kutokea katika kanisa la Hantoukoura nchini Burkina Faso.

 

Waathirika wa shambulio hilo walikuwa wamehudhuria katika ibada ya jumapili , mashariki mwa nchi hiyo.

Eneo hilo ambalo wanamgambo wa kiislamu wamechukua limekuwa na migogoro tangu mwaka 2012 kabla ya jeshi la Ufaransa kuwaondoa.

Mamia ya watu wameuwawa katika taifa hilo miaka ya hivi karibuni huku kundi la kigaidi la jihadist likidaiwa kuhusika na mauaji hayo, kutokana na mvutano wa kikabila na kidini haswa katika mpaka wa Mali.


Loading...

Toa comment