The House of Favourite Newspapers

Watu 7 wafariki baada ya fuso na tenka la mafuta kugongana Moro

accident2-415x260

WATU saba wamepoteza maisha huku mwingine mmoja akijeruhiwa vibaya baada ya lori lililokuwa likisafirisha nyanya aina ya fuso kugongana na tenka la mafuta katika eneo la Fulwe, Mikese kwenye barabara kuu ya Morogoro – Dar es Salaam jana ambapo miongoni mwa waliokufa ni madereva wa magari yote mawili.

Ajali hiyo ilihusisha lori aina ya fuso lenye namba za usajili T 153 ASC mali ya Felician Kinguza, lililokuwa na shehena ya nyanya, likitokea Msowero wilayani Kilosa, kuelekea jijini Dar es Salaam likiendeshwa na dereva aliyetambulika kwa jina moja la Patrick, ambalo limegongana na tenka la mafuta aina ya Scania, mali ya Mlay, majira ya saa nane usiku, ambapo inadaiwa fuso lilijaribu kulipita gari dogo aina ya Corola na ghafla dereva alikutana na tenki na kugongana hivyo kusababisha ajali hiyo.

Taarifa kutoka eneo la tukio zimebainisha kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa lori aina ya fuso.

Comments are closed.