The House of Favourite Newspapers

Wazee wa Yanga Wazidi Kumkaba Koo Manji (Picha&Video)

akilimali-1

Katibu wa Kamati ya Muafaka ya Wazee wa klabu hiyo, Ibrahim Akilimali akizungumza na wanahabari.

akilimali-2

Wanahabari wakichukua tukio hilo.

WAZEE wa Klabu ya Yanga wakiongozwa na Katibu wa Kamati ya Muafaka ya Wazee wa klabu hiyo, Ibrahim Akilimali, wamezidi kumkalia kooni mwenyekitiwa klabu hiyo,Yusuf Manji kutokana na nia yake ya kutaka kuikodisha Yanga na nembo yake kwa muda wa miaka kumi.

Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Mzee Akilimali alisema kuwa: “Hatutaki kurudi kule tulipokuwepo katika mgogoro wa miaka saba, mwaka 2003 ndiyo tukapata usuluhisho na kukubaliana kuwa litumike jina ambalo lilikubaliwa na waasisi wetu, tukakubaliana kuwa kuwe na Yanga SC na Yanga Cooperation,
“Yanga kampuni ilifikishwa na kukawa na utaratibu kuwa kuwe na hisa, Yanga SC kuwe na hisa 51 na wanachama wawe na asilimia 49, na tulizunguka mikoa mingi ili kufuta mgogoro uliokuwepo na kuomba ridhaa ya wanachama wa klabu kukubali hisa.

“Tulipata mwenyekiti mpaka anatoka timu ilikuwa na Mil. 200, tukampata Bwana Nchunga yeye akajiuzulu baada ya miaka miwili, tukamchagua Bwana Manji akaongoza kwa miaka miwili, kwasababu tu ya upenzi akaongeza muda, ili tujipange na yeye ajipange na baadaye tukafikia hatua ya kumchagua kwa mara nyingine.
“Haijafika hata miezi nane imeibuka swala la deni la bilioni 11 na laki sita, jambo ambalo limetushtua Wanayanga, limekuja tamko la mwenyekiti kuleta hoja kuwa akodishwe Yanga na nembo yake kwa muda wa miaka 10, kwasisi wote tunasema Yanga ni kubwa, Yanga haiwezi kukodishwa.

“Kupitia mimi na wazee wa kamati tumesema hatukubaliani na hilo.”
Naye mwanachama wa klabu hiyo aliyekuwa ameambatana na Akilimali, Mohammed Msumi, alisema kutokana na Manji kuwa na mahitaji makubwa na klabu ni vyema akakaa pembeni na kuanzisha timu yake mwenyewe na kuacha Yanga iendeshwe na mfumo ambao umezoeleka.

Na Denis Mtima/GPL

Comments are closed.