The House of Favourite Newspapers

Waziri Mkuu Mdogo Zaidi Duniani na ‘Kisu’

0

SANNA MARIN wa Finland  ndiye waziri mkuu mwenye umri mdogo zaidi duniani baada ya kushika wadhifa huo nchini humo akiwa na miaka 34.

 

Marin alichaguliwa na chama chake cha Social Democratic baada ya kiongozi wa chama hicho ambaye pia alikuwa waziri mkuu, Antti Rinne, kujiuzulu wiki iliyopita.

Kabla ya kuwa waziri mkuu, Rinne alikuwa waziri wa uchukuzi na mawasiliano nchini Finland tangu mwezi Juni mwaka huu,  hivyo amehudumu kwa miezi sita pekee. Marin anatarajiwa kuapishwa wiki hii.

Marin ambaye ni waziri mkuu wa tatu mwanamke nchini Finland, atakuwa amevunja rekodi ya kuwa waziri mkuu mdogo zaidi duniani ambapo Waziri Mkuu wa New Zealand,  Jacinda Ardern, ana miaka 39, na Waziri Mkuu wa Ukraine, Oleksiy Honcharuk ana miaka 35.

 

Leave A Reply