The House of Favourite Newspapers

Wema afungukia ugomvi wake na Aunt

0

wemanaauntWema Sepetu na Aunt Ezekiel.

IMELDA MTEMA, Amani

STAA wa filamu Bongo, Wema Sepetu amefungukia ugomvi ambao hutokea mara kwa mara na shosti wake ambaye pia ni muigizaji, Aunt Ezekiel usiingiliwe na mtu kwani wanapogombana tofauti zao wanazimaliza wenyewe na si mtu mwingine yeyote.

Akizungumza na Amani Wema alisema kuwa, yeye na Aunt ni watu waliopo karibu sana na wanaopendana hivyo inapotokea wanagombana huwa ni kitu kidogo kwao kwani huyamaliza na maisha yanaendelea kama kawaida.

“Jamani nyinyi mtuache tu, tunatibuana na Aunt, tunajuana vizuri sana ugomvi wetu ni wa mara kwa mara lakini tunamalizana wenyewe kwa sababu ukweli ni kwamba hatuwezi kukaa mbalimbali kwa muda mrefu kutokana na kupendana,” alisema Wema.

Leave A Reply