The House of Favourite Newspapers

Young Dee Aachia Wimbo wa Kumfariji Dogo Janja Baada ya Kufiwa na Baba Yake Mzazi

young-dee1Msanii wa muziki wa hip hop hapa nchini, Young Dee amesema ameachia wimbo uitwao, ‘Furaha’ ambao ni maalum kwa ajili ya kumfariji msanii wenzake Dojo Janja aliyefiwa na Baba yake mzazi, juzi jumapili nyumbani kwao mkoani Arusha.

Janjaro2_NoizRapa huyo ambaye alikuwa kimya kwenye muziki tangu atangaze kuachana na matumizi ya Madawa ya kulevya, amedai hakuwa na mpango wa kuachia wimbo huo.

Dogo Janja Afiwa na Baba yake Mzazi

Kupitia Instagram, Young Dee ameandika:

Nilipanga kuachia video yangu nikiwa na furaha sana. Furaha yangu nilitamani sana itawale kwanzia kwangu, mashabiki wangu, pamoja na wasanii wenzangu. Bahati mbaya msanii mwenzangu @dogojanjatz amepoteza nguzo imara sana katika maisha yake. Miaka 8 iliyopita nilipitia changamoto kama hiyo kwa kumpoteza mzee wangu. Kitu pekee nilichokua nahitaji ni FURAHA itokanayo na faraja kutoka kwa watu walionizunguka. Nilikua sina mpango wowote wa kuachia wimbo wangu wiki hii. Lakini nimeamua kuachia Video ya wimbo wangu leo, kama Dedication kwa @dogojanjatz. Wimbo wangu unaitwa FURAHA. Naamini ni nguzo pekee anayoihitaji Mwanangu Janjaro kwa sasa. You Have all my Support Young Badman, I have Nothing But Love to You.

 

Nilipanga kuachia video yangu nikiwa na furaha sana. Furaha yangu nilitamani sana itawale kwanzia kwangu, mashabiki wangu, pamoja na wasanii wenzangu. Bahati mbaya msanii mwenzangu @dogojanjatz amepoteza nguzo imara sana katika maisha yake. Miaka 8 iliyopita nilipitia changamoto kama hiyo kwa kumpoteza mzee wangu. Kitu pekee nilichokua nahitaji ni FURAHA itokanayo na faraja kutoka kwa watu walionizunguka. Nilikua sina mpango wowote wa kuachia wimbo wangu wiki hii. Lakini nimeamua kuachia Video ya wimbo wangu leo, kama Dedication kwa @dogojanjatz. Wimbo wangu unaitwa FURAHA. Naamini ni nguzo pekee anayoihitaji Mwanangu Janjaro kwa sasa. You Have all my Support Young Badman, I have Nothing But Love to You. Link on my Bio..

A video posted by PAK👁RAPPER (@youngdaresalama) on

Young Daresalama – Furaha (Official Music Video)

Comments are closed.