The House of Favourite Newspapers
gunners X

Mwili wa Balozi Kijazi Waagwa UDOM – Video

0

MWILI wa aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Eng. John Kijazi, aliyefariki dunia jana Jumatano saa 3:10 usiku katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, unaagwa leo Alhamisi, Chuo Kikuu cha Dodoma. Kijazi, alikuwa pia mkuu wa chuo hicho.

Baada ya kuagwa utasafirishwa leo Februari 18 kwenda Dar es Salaam ambako ibada nyingine ya kuuaga itafanyika kesho Karimjee jijini Dar es Salaam na baadaye kusafirishwa kwenda Tanga ambapo siku ya Jumamosi utazikwa wilayani Korogwe mkoani Tanga.

Katibu Mkuu-Ikulu, Moses Kisiluka,Β  amesema, Rais John Magufuli kesho Ijumaa, ataongoza shughuli ya kuuaga mwili huo katika viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam.

 

 

 

 

Leave A Reply