Harmo: Shoo ya Yanga Sishindani na Mtu, Mtashangaa – Video

 

MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Harmonize amefunguka kuwa shoo yake atakayoifanya  Uwanja wa Mkapa kwenye kilele cha Sherehe ya Wiki ya Wananchi itakuwa shoo ya kihistoria ambayo haijawahi kufanyika nchini.

 

Harmonize amesema hayo leo Jumanne, Agosti 25, 2020, jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wanahabari kwenye hafla ya uzinduzi wa msimu wa pili wa Sayona Twist ambaye  ndiye balozi wa kinywaji hicho.

 

“Watu wanauliza kwamba Harmonize ataingia pale Taifa (Uwanja wa Mkapa kwenye Tamasha la Kilele cha Wiki ya Wananchi, Yanga SC), mimi sipendi kusema maneno mengi sana, lakini hii itakuwa best performance ever.

 

“Ninawashukuru media zote, Global TV Online, (anataja na media nyingine zilizohudhuria). Leo nitaanza rehearsal pale Uwanja wa Taifa (Uwanja wa Mkapa), nawakaribisha mkiwa na muda mje kuona maandalizi ya shoo ya mapinduzi ya burudani.

 

“Mimi kushabikia Yanga SC sio dhambi wala siyo ugomvi, na siamini kama mtu akishabikia timu flani itampunguzia mashabiki, nachofanahamu michezo si uadui, ni furaha na urafiki, lakini muziki ni biashara, wakati mwingine hizi ni mentality tu za watu, mimi sifanyi kushindana na mtu.” amesema Harmonize.

 

Toa comment