The House of Favourite Newspapers

JPM: Napenda Nifike Mbinguni, Niwe ‘Waziri wa Malaika’ – Video

0

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na mgombea urais kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, kupitia chama hicho,  Dkt. John  Magufuli,  amesimama na kuzungumza na wananchi wa Iramba mkoani Singida katika kampeni zake wakati akielekea mkoani Tabora leo, Jumatano, Septemba 2, 2020, akiwa katika mwendelezo wa kampeni zake kuwania nafasi hiyo.

 

Akihutubia katika mkutano huo, baadhi ya maneno aliyosema Magufuli ni haya;

“Hapa Misigiri hapakuwa na umeme wa namna hii, hata mitandao ya simu haikuwepo, tumejenga vituo vya afya, tumesambaza umeme maeneo mbalimbali, nitashangaa watu wa Singida mkisema hatujafanya kitu chochote, lazima tujiulize tulikotoka, tulipo na tunakoelekea.

 

“Wapo wenye maneno matamu, watawaahidi kila kitu, ukiwa unatafuta mwanamke sisi wanaume huwa tunadanganya sana… Mimi nitakununulia vitenge, nina biashara zangu Mwanza… Kumbe hata nyumba hana? Unamuacha uliyehangaika naye unaenda kuteseka mnalala kwenye ngozi.

 

“Nawaomba ndugu zangu tuangalie maendeleo tangu Mwl. Nyerere, Mzee Mwinyi, Mzee Mkapa, Mzee Kikwete, na mimi kwa miaka mitano nimefanya mabaya yote ndugu zangu? Nani hajui hata hii lami haikuwepo, tulikuwa tunapita Mlima wa Sekenke, watu wamekufa pale.

 

“Nimezungumza hadharani mmenisikia, ndiyo maana nikasema wewe gombea hapa (Dkt. Mwigulu) na wewe nenda Ubungo (Prof. Kitila) kwa sababu amekaa pale kwa miaka 20, wote ninawahitaji na ninataka wote washinde, mimi najua nitafanya nini juu yao.

 

“Nimekuja kuwaomba kura kwa sababu tuliyoyafanya tumefanya pamoja na ninyi, siwezi kuliacha taifa hili liangamie, liingie kwenye mikono ya watu matapeli, watu waongo, nataka niliache taifa hili kwenye mikono salama.

 

“Mimi sitoi ahadi za uongo sababu msema kweli ni mpenzi wa Mungu… Sitaki nitende dhambi kwa kuwaambia wazee wangu ya uongo, ninapenda na mimi siku moja nifike mbinguni, malaika waseme ulifanya mazuri, tunakupa sasa hata kauwaziri wa Malaika”

 

Leave A Reply