Chongolo: Upatikanaji wa Maji Mjini ni 86% – Video

KATIBU  Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo, amesema kwamba baada ya miaka 60 ya Uhuru, upatikanaji wa maji katika miji umeongezeka hadi kufikia asilimia 86.

 

Kauli hiyo ameitoa hii leo Desemba 8, 2021, Dar es Salaam, wakati akizungumzia mafanikio yaliyopo baada ya miaka 60 ya Uhuru, wapi walikotoka na wapi ilipo serikali inayoongozwa na chama hicho, huku akiahidi kwamba chama hicho kitaendelea kujenga Tanzania imara katika nyanja mbalimbali za amendeleo.

 

“Leo hii tunapozungumzia tunu za Taifa zikiwemo za amani, umoja, mshikamano, uzalendo na utulivu katika nchi, vyote vimesimamiwa na CCM kuanzia enzi za TANU na ASP,”

 

“Nchi yetu wakati inapata Uhuru, upatikanaji wa maji katika miji yetu ulikuwa kwa asilimia 25 tu kuna miji ilikuwa inapata maji kwa asilimia 8, 6 ama 10, lakini leo miaka 60 baada ya Uhuru upatikanaji wa maji ni asilimia 86, tuko kwenye kiwango kizuri,” amesema Chongolo.

 

“CCM tunaposimama kuzungumzia umuhimu wa miaka 60 ya Uhuru tunazungumzia suala ambalo tunawajibu nalo kwa 100%, ikizingatiwa kuwa chama hiki ndicho kimepewa dhamana ya kuongoza nchi na kilipewa dhamana hiyo na wananchi,” amesema Daniel Chongolo.


Toa comment