The House of Favourite Newspapers

Magufuli: Hakuna Uzazi wa Mpango, Fyatueni Watasoma Bure – Video

0

MGOMBEA urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),   Dkt. John  Magufuli leo alikuwa, katika Uwanja wa Bombardier Singida Mjini ambako alifanya mkutano wa kampeni, ikiwa ni miongoni mwa vituo vya kampeni zake alizofanya leo, Septemba 1,  2020 

 

Baadhi ya kauli alizozitoa kwenye kampeni zake hizo ni:

“Mimi siwezi kusema mkinichagua kodi nitafuta, utaendeshaje nchi, siwezi kufuta kodi. Hata Ulaya wanalipa tena wana sheria kali kweli, tutaendelea kulipa kodi inayowezekana, ndiyo maana Wamachinga tumewawekea kodi ya Sh 20,000 kwa mwaka.

 

“Kuna watu wanasema tutafanya hivi, tutafanya vile, hizo ni ndoto, kuongoza nchi si mchezo ni kazi kubwa, huwezi kusema mimi mkinichagua kila kitu nitawaletea na wala huwezi sema mimi mkinichagua hamtolipa kodi, utaendeshaje nchi bila kodi?

 

“Nchi hii ilikuwa shamba la bibi, kila mahali tulikuwa tunaibiwa. Tena hata Watanzania wenzetu walikuwa wanatetea wezi. CCM imeweka umeme kwa vijiji 9,570 ndani ya miaka mitano na haiwezi kushindwa vichache vilivyobakia.

 

”Kila mmoja atupigie kura, sababu maendeleo hayana chama, kwani taa za barabarani CCM haziwamulikii? ACT haziwamulikii? Chadema haziwamulikii? CUF haziwamulikii? Zinawamulikia mpaka paka wanaokatiza mle usiku, tunataka maendeleo kwa wote.
“Hata majirani zetu wanateseka sana kisa corona, niwaombe watu wa duniani watambue Mungu yupo. Viongozi wa dini endeleeni kuwafundisha watu wa mataifa wajue Mungu ndio kila kitu.  Tulivyobanana hapa si tungekufa wote ila corona, imekoronea mbali kwa sababu tulimuamini mungu.
“Nchi yetu kuna wengi sana wanaionea wivu, hatuna corona, tumeingia uchumi wa kati, wakati nyingine uchumi unashuka kisa corona, ripoti ya mwaka 2020 ya Global Peace Index inasema Tanzania ni mahali penye usalama zaidi tunaongoza Afrika Mashariki, wale wabishi wakatazame mtandaoni.
“Mkinichagua tena nawahakikishia vijiji vyote Tanzania vitakuwa na umeme, siwezi kuwadanganya na jua linawaka, na mimi nataka niuone ufalme wa Mungu nitakapotoka duniani, ahadi zote nitatekeleza.
“Kama tulivyoshikamana wakati wa corona na wakati huu wa kampeni tuwe pamoja, tuijenge amani yetu, akipita mtu anawaambia ‘mpaka kitaeleweka,tutapigana’ tumuogope sana, sisi ni wamoja unaweza kumpenda binti ni CHADEMA wewe ni CCM mkaoana, kwani mapenzi yana vyama? Hayatonoga?
“Tunataka watoto wasome bure, ndiyo maana siku zote nilisema zaeni hakuna kuzaa kwa mpango, matiti ya kunyonyesha watoto tunayo, maziwa tunayo na wanaume wapo, wakina mama wapo na shule wanasoma bure, serikali ipo,” amesema Magufuli.”

Leave A Reply