JPM: Msichague Upinzani Watafuta Miradi Yetu – Video

 

MGOMBEA urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),  John Magufuli amewataka wananchi wa Usagara, wilaya ya Misungwi kukiamini chama hicho na kuwachagua wagombea wa CCM ili wakaendeleze kazi waliyoianza badala ya kuwachagua upinzani.

 

Amesema hayo leo Jumanne, Septemba 8, 2020, wakati akizungumza na wananachi wa Usagara, Mwanza, akivuka kuelekea Sengerema kuendelea na kampeni zake.

 

“Babu yangu alikuwa anaitwa Michael Nyahinga Ng’wanang’ombe Bulahya, alikuwa katekista katika Kigango cha Nyasubi, na pale kuna kaburi la shangazi yangu. Baba wa babu alizikwa Kijiji cha Ng’ombe, hivyo wengine hapa ni ndugu zangu, ndiyo maana nilishindwa kuoa hapa Misungwi nikaenda kuoa Nguge.

 

“Ninaomba mtuamini, mwendelee kuiamini CCM, mnaona kazi ambayo tunaifanya pale kwenye Daraja la Kigongo – Busisi, lenye urefu wa kilomita 3.2.

 

“Msichague wengine wakaja kufuta hii miradi kama daraja la Kigongo – Busisi, limegaharimu Tsh bilioni 699, haya mambo ya siasa wasiwatenganishe. Bahati nzuri hata ndoa ya Mnyeti aliyeiandaa ni Mheshimiwa Kitwanga, nampongeza Mnyeti kwa kuteuliwa,” amesema Magufuli.

 

Toa comment