The House of Favourite Newspapers

Magufuli: Kimbunga cha Leo Mwanza Sitakisahau – Video

0

MGOMBEA Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), leo Jumatatu, Septemba 7, 2020, yupo katika Uwanja wa CCM Kirumba kuhutubia mkutano wa hadhara wa kampenzi zake za urais jijini Mwanza.

 

Miongoni mwa mambo aliyoyasema ni yafuatayo:

“Nimefurahi sana kuukuta Uwanja wa CCM Kirumba umejaa wote, kuanzia sehemu ambayo wanamichezo huwa wanachezea mpaka kwenye viti, na wengine wameshindwa kuingia wapo nje, ni upendo wa dhati, hii ni dalili nzuri ya ushindi, wanaojitokezatokeza wataisoma namba.

 

“Nilikuwa natoka Igogo, napita Bugando, Mwanza Seco, Mtaa wa Rufiji mpaka shuleni Lake Secondary. Kila siku nilikuwa natembea kwa miguu, nimeishi Kitangiri wakati nafanya kazi na mke wangu alikuwa anafundisha Shule ya Msingi Kitangiri, Mwanza ninajiona ni nyumbani.

“Katika suala la kuboresha elimu tumekarabati Shule za Sekondari; Nganza, Bwiru Boys, Bwiru Girls, Pamba, Mwanza na Chuo cha Walimu, Murutunguru Ukerewe. Tumeanza ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma na juzi tumetangaza tenda ya kuanza kujenga Standard Gauge kutoka Mwanza kwenda Isaka kilomita 250.

 

“Tunaupanua uwanja huu wa Mwanza, ndege yoyote kutoka nchi yoyote itatua hapa, tuongeze watalii, tukuze uchumi wetu. Wapo wanaobeza atapigiwa kura na madaraja, hao wanaobeza wafundisheni siku ya uchaguzi, watu wanaopita kwenye hayo madaraja kama la Furahisha, wanaotibiwa kwenye hospitali tulizojenga, watanipigia kura Oktoba 28.

“Kwenye bajeti ya mwaka huu, tumetenga shilingi bilioni 15 kwa ajili ya kufanya ukarabati mkubwa wa meli zingine ikiwepo meli kubwa ya MV Umoja iweze kuwa inabeba mabehewa mengi zaidi.

 

“Mtu anaweza akasimama akasema ndege hazina faida; aje awaulize wavuvi wa Mwanza ambao wanavua masamaki, wanapata mabondo pamoja na minofu inaposafirishwa kwa urahisi kwenda Ulaya wanatengeneza pesa.

 

“Nimefurahi sana wananchi wa Mwanza, kimbunga kilichotokea hapa sitakisahau maishani mwangu, tunashukuru sana kwa sababu mmetuamini, mmetuonyesha upendo wa pekee. Nawaomba CCM, ACT, Chadema, vyama vyote na msio na vyama, Oktoba 28 mtupatie kura za kishindo.”

 

 

Leave A Reply