The House of Favourite Newspapers

Magufuli: Shigongo Ameanza Kunisumbua, Nampa Lami – Video

0

MGOMBEA urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),  John Magufuli, ameahidi kujenga barabara ya kutoka Sengerema, Nyehunge mpaka Kahunda kwa kiwango cha lami katika kipindi kijacho cha miaka mitano iwapo atachaguliwa tena kuiongoza Tanzania.

 

Magufuli ametoa ahadi hiyo  hayo leo Jumanne, Septemba 8, 2020, wakati akizungumza na wananchi wa Bukokwa na Nyehunge katika Jimbo la Buchosa mkoani Mwanza, wakati akiendelea na kampeni zake mkoani humo.

 

“Sikuwa nimepanga kupita Buchosa, jana tulipomaliza mkutano Mwanza, Shigongo akaanza kunipigia simu, nikamwacha nikijua ana mambo yake, akampigia msaidizi wangu, akamjulisha RC Mwanza nataka Mheshimiwa Rais apite kwenye bararabara ya changarawe, ili nikimuomba aione.

 

“Bibi yangu na babu yangu nimewazika Katoma, nimebatizwa hapa Kalebezo, maeneo yote ya Buchosa nayafahamu, ninawafahamu ndugu zangu, kazi yangu kubwa nikuwaletea maendeleo.

 

“Kwenye mchakato wa Jimbo la Buchosa ulikuwa wa demokrasia, kura za Eric Shigongo na za Dkt. Tizeba zilifungana, tukakuta Tizeba alikuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu hivyo alijipigia kura tukaitoa, akawa wa pili tukampitisha Shigongo, uongozi ni kuachiana.

 

“Tizeba amefanya mengi kwenye Serikali kwa miaka yake kumi, kazi zipo nyingine tu tutampa atusaidie sehemu kwenye Serikali, sasa ni muda wa Shigongo mpeni kura, na ameshaanza kunisumbua lami nimeshindwa hata kusema lakini nitaijenga tu, mniachie mimi.

 

“Luchili palikuwa na madaraja ya mbao, kutoka Sengerema, Nyehunge mpaka Kahunda (takribani Km 47), hii barabara tutaijenga kwa kiwango cha lami, acheni ubaguzi na kupigana vita, mpeni kura Shigongo, kama Tizeba amenyoosha mkono na kumpa kura Shigongo, unayekataa ni mchawi.

 

“Barabara ya Sengerema – Nyehunge tutaijenga kwa lami, lakini labda tuipitishe kule pembeni sababu mmejenga karibu na barabara hapa Bukokwa, sheria inasema mita 30 kutoka katikakati ya barabara, kama tutaipitisha hapa mnapotaka hizo nyumba hakuna fidia.” -Dkt. Magufuli, Bukokwa.

 

Leave A Reply