The House of Favourite Newspapers

Magufuli Atua Sengerema Aahidi Mazito – Video

0

MGOMBEA urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John  Magufuli anaendelea na mikutano yake ya kampeni na leo Jumanne, Septemba 8, 2020, anafanya mkutano wake katika Uwanja wa Mnadani, Sengerema mkoani Mwanza.

 

“Sengerema mimi ni nyumbani, nilianza maisha yangu ya kufanya kazi Sengerema Secondary miaka ya 1982-1984, hata lami haikuwepo, kulikuwa na changarawe, basi moja tu la Digidigi nalo lilikuwa linapita mara moja kwa wiki, hivyo Sengerema naijua.

 

“Mradi mkubwa wa maji Sengerema – Nyamazugo umegharimu zaidi ya Tsh bilioni 22 na miradi mingine ya maji mingi hapa, hii ni kuhakikisha shida ya maji tunaifuta hapa Sengerema.

 

“Tumebana pesa kutoka kwa mafisadi tumejenga hili Daraja la Kigongo – Busisi, hili daraja litaleta maendeleo makubwa na kukuza uchumi hapa Sengerema, nyie ndiyo mashahidi, msichague mwingine anaweza kuchukua vyuma vile akauza skrepa; uongozi haujaribiwi.

 

“Tulimwamini Mungu na tukamwomba, corona ikapita, hatukuwa na cha lockdown, tuliruhusu watu walime, wachape kazi, wananchi wa Sengerema wamelima na wamevuna mazao mengi, nawaomba msiuze mazao yenu ovyo mtapata njaa, uza mazao kama tayari umeshavuna mengine.

 

“Katika sekta ya afya, tumejenga hospitali mbili za Wilaya Sengerema na Buchosa, tumejenga vituo vya afya vitano; Kagunga, Kamanga, Nkome, Nyakaliro na Katunguru. Ndiyo maana tunaomba muendelee kutuamini.

 

“Huyu Tabasamu mimi namfahamu vizuri, ana upendo wa dhati kwa Sengerema, ana uchungu na Sengerema, kama lilivyo jina lake na anavyotabasamu atawaletea maendeleo ya kweli, nileteeni huyu na madiwani wa CCM.

 

“Nafahamu mna ombi la barabara ya kutoka Sengerema, Nyamazugo mpaka Nyehunge (Km 54.67), ngoja nilipite hili barabara leo nikifika Nyehunge nitalizungumzia hukohuko, kwa sababu na mbunge mtarajiwa wa Buchosa, Mheshimiwa Shigongo tunaye hapa, nafahamu mna ombi la kivuko kipya cha Kahunda – Maisome, kilichopo sasa hivi MV Tegemeo kimeanza kuharibika, haya tutayaongea Buchosa,” amesema Magufuli.

 

Leave A Reply