The House of Favourite Newspapers

JPM Akichukua Fomu Urais: Tutakampeni Kistaarabu – Video

0

MWENYEKITI  wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais John Magufuli, leo  6, 2020, l amechukua fomu ya kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM katika Ofisi za Makao Makuu ya Tume ya Taifa ya UchaguziTanzania (NEC) Njedengwa jijini Dodoma.

 

Magufuli amechukua fomu majira ya saa 3 asubuhi na akasindikizwa na watu wachache wakiwemo viongozi wakuu wa CCM, ikiwa ni kutekeleza matakwa na maelekezo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

 

Magufuli anachukua fomu hiyo ili kugombea urais kwa kipindi cha pili katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 28 Oktoba, 2020.

 

 

Baada ya kuchukua fomu,  Magufuli alikwenda katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM jijini Dodoma (White House) na kukutana na wanachama, wapenzi na wakereketwa wa CCM na kuwasalimu.

 

“Tutafanya kampeni kwa kumtanguliza Mungu. Naamini atatulinda kama alivyotulinda na corona. Leo Tanzania hatuna corona, ndiyo maana tunabanana tu hapa na hata vitandani muendelee kubanana tu.

 

“Mimi na Mama Samia (Mgombea-mwenza) tutafanya kampeni za ustaarabu sana. Tutaheshimu watu wote na naamini watu wa vyama vyote watatupigia kura kwa sababu maendeleo hayana chama.

“Mtu akisema nitapigiwa kura na vituo vya afya najua ndiyo wameshaanza kunipigia kampeni hivyo, maana vituo vya afya wametibiwa wanawake watanipigia kura. Wazee hata walevi walilala humo watanipigia na inanipa nguvu kuwa ushindi wa mwaka huu utakuwa mkubwa.

 

“Wakati tunaingia madarakani, nchi yetu ilikuwa na vijiji 3,000 tu vilivyokuwa na umeme lakini sasa vimefika 9,402 na tumebakisha vijiji kama 3,000 kumaliza vyote.

“Sasa tukipewa miaka mitano tena tushindwe kumaliza vijiji hivyo. Ndiyo maana nikasema lazima niombe kura ili nikamalizie kiporo kikubwa kilichobaki, kwa sababu najua fedha tutapata wapi, tutabana wapi na ni mafisadi gani watazitapika ili ziende kutumika kwa ajili ya wananchi.

 

“Wanachama wa CCM msitembee tu mkisema Magufuli ameshinda au chama kimeshinda, naomba mjitokeze kupiga kura. Msipopiga kura maana yake hizo kura mnazipunguza. Napenda kuwathibitishia nimeomba hii nafasi si kwa kulazimishwa ila nataka kuwatumikia wanyonge,” amesema.

 

Leave A Reply