The House of Favourite Newspapers

Lwandamina Awahenyesha Msuva, Niyonzima Kwenye Jua Kali Zenji

lwandamina-4
Musa Mateja na Said Ally, Championi Jumatano Toleo na 1955

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mzambia, George Lwandamina, kuonyesha kuwa hataki mchezo katika kikosi hicho jana Jumanne, aliwahenyesha wachezaji wake kwa kuwafanyisha mazoezi kwenye jua kali.

Lwandamina aliyafanya hayo ikiwa ni siku moja tu baada ya Yanga kuwabanjua Jamhuri kwa mabao 6-0 katika mchezo wa Kombe la Mapinduzi linaloendelea visiwani Zanzibar.
Mabao ya Yanga katika ushindi huo yalifungwa na Simon Msuva na Donald Ngoma walofunga mawili kila mmoja, Thabani Kamusoko na Juma Mahadhi ambao waliingia nyavuni mara moja kila mmoja.
Mazoezi hayo yaliyofanyika katika Uwanja wa Kiyanga, Mkoa wa Mjini Magharibi yalikuwa mahususi kwa ajili ya kujiwinda na mchezo wa leo wa kikosi hicho ambacho kitawavaa Zimamoto.

NIYONZIMA (7)
Tangu atue ndani ya kikosi hicho akitokea Zesco ya Zambia, Lwandamina amekuwa akisifika kwa kutoa mazoezi magumu kwa wachezaji wake ambapo lengo lake ni kuhakikisha wanakuwa na stamina ya kutosha kwa ajili ya kukabiliana na mikikimikiki ya Ligi Kuu Bara pamoja na Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo Yanga watawavaa Wacomoro, Ngaya Club.
Wengi waliona kama ni kitu cha ajabu kwa timu hiyo kufanya mazoezi hayo jana asubuhi kwa kuwa walitoka kwenye mechi usiku na walitegemea kuwa wangefanya jioni.
Mazoezi hayo yaliyosimamiwa na Lwandamina pamoja na wasaidizi wake, Juma Mwambusi na Noel Mwandila yalianza saa tano asubuhi na kumalizika saa saba mchana.

halotel-strip-1-1

Comments are closed.