Mkwere Amwaga Machozi Harusi ya Masele Chapombe Siku ya Ndoa Yake

Msanii maarufu wa vichekesho anayetamba na Kundi la Vichekesho la Mizengwe, linalorusha kipindi chao kupitia runinga ya ITV, Hemed Maliyaga ‘Mkwere’, amemwaga machozi ukumbini wakati wa sherehe ya rafiki yake wa kushibana, Crispine Lyogello ‘Masele Chapombe’ ambaye amefunga ndoa ya kanisani na kufuatiwa na tafrija ya nguvu katika Ukumbi wa Mbezi Luxury.mkwere3

Mkwere katika pozi.

Mkwere alishindwa kuyazua machozi wakati alipoombwa ukumbini kutoa ujumbe wowote siku ya harusi hiyo, ambapo alianza kusimulia historia yake na Masele huku machozi yakimtoka.  Mkwere alisema yeye na Masele wamekuwa wakishirikiana tangu wakiwa wanatafuta maisha ambapo walisota sana lakini wakakaza mikanda hadi kufikia mafaniko ya kujulikana katika tasnia ya komedi nchini.

Urafiki wao, kwa mujibu wa Mkwere, ulizileta karibu familia mbili za watu hao maarufu nchini kwa maigizo.masele-chapombe-6

Masele na Mkewe.

 

 

????????????????????????????????????

Mkwere

mkwere1

masele-27Wakiwa ukumbini, Mkwere alisema alikumbuka mambo mengi tangu walipoanza kutafuta maisha kupitia sanaa.

masele-22Mkwere akimkumbatia Masele

“Masele ni rafiki yangu sana, nimetoka naye mbali, nakumbuka nilikuwa nalala kwao hata wiki nzima ili asubuhi tuwahi ITV kwa miguu kwa ajili ya kutayarisha kipindi.

“Masele ndugu yangu, umekua kama nilivyokua mimi, tupigane kwa ajili ya familia zetu, kuanzia sasa tufanye kitu kipya ambacho kitakuwa tofauti kwa familia zetu na taifa kwa jumla,” alisema Mkwere huku akiangua kilio.

mkwere4

Mkwere na mwanae.

masele-24

Naye mama mzazi wa Masele, Jane Lyogello, alisema: “Masele aliponiambia anataka kuoa, nilishangaa, nikajua ananileta sanaa yake lakini kumbe alikuwa amedhamiria na ninamshukuru Mungu tumekamilisha suala lake.”

Sherehe ilichangamka kwa vituko vya hapa na pale hasa vya ucheshi ambapo mara baada ya kupigwa wimbo wa Darassa uitwao  ‘Muziki’,  uvumilivu ulimshinda Masele na kujikuta akianza kucheza kwa staili ya kulewalewa.

Baadhi ya wasanii waliojitokeza katika hafla hiyo mbali na Mkwere ni pamoja na Erick Kisauti, Kondo Msambaa na wengine ambao waliichangamsha vilivyo shughuli hiyo.

Salum Milongo/GPL


Toa comment