Ndoa ya Masele Yampa Wakati Mgumu MC Pilipili

pilipili-4Mc Pilipili.

Mchekeshaji na mshereheshaji  (MC) bora wa mwaka 2017 aliyeshinda tuzo ya Instagram Party, Emmanuel Mathias ‘MC Pilipili’, ameshindwa kuweka wazi ni lini atafunga ndoa na mchumba wake, Rose Ndauka, kufuatia mchekeshaji Crispin Lyogello ‘Masele Chapombe’  kuingia mwaka 2016 kwa kuuaga ukapera.   masele-13

Masele na Mkewe

MC Pilipili amekuwa akiweka picha mara nyingi katika mitandao ya kijamii zinazomuonyesha yeye na mchumba wake huyo  wakiwa mapumzikoni. Rose amezua hali ya utata juu ya taarifa hiyo kwani mara tu baada ya shoo kubwa iliyofanyika Decemba 25 2016 Dodoma, Rose hakuweka picha yoyote ikiwaonyesha wawili hao katika mitandao ya kijamii.

pilipili-3  Pilipili ameendelea kuweka picha zinazoonyesha familia yao, yaani yeye, Rose na mtoto wa Pilipili aitwaye Mariam Emmanuel Mathias.img-20170110-wa0003Rose Ndauka na Mc Pilipili

img-20161228-wa0031 Paliwahi kuenea video fupi katika mitandao ya kijamii ikimuonyesha mchekeshaji Emmanuel Masanja akimchapa viboko Emmanuel Mathias  (MC Pilipili) kwa kudai kwa nini mpaka hii leo bado hajaoa ambapo MC huyo ameahidi mwaka huu anaweza kufanya chochote katika suala hilo la ndoa.

Salum Milongo/GPL

 


Toa comment