Rais Museveni Amteua Mwanaye Kuwa Mshauri Wake
RAIS Yoweri Museveni wa Uganda amemteua mwanaye, Meja Jenerali David Muhoozi Kainerugaba, kuwa mshauri mkuu wake kuhusu operesheni maalum.
Rais Yoweri Museveni.
Jenerali Kainerugaba amekuwa kamanda wa kikosi maalum cha wanajeshi (SFC) chenye jukumu la kutekeleza operesheni maalum za kijeshi. Kikosi hicho husimamia ulinzi wa rais na kulinda maeneo muhimu kwa serikali nchini Uganda.
Rais Yoweri Museveni.
Rais Yoweri Museveni.
Katika uteuzi ambao hufanywa na Museveni katika serikali yake, mke wake, Bi Janet Kataaha Museveni, ni Waziri wa Elimu na Michezo, wadhifa ambao alipewa Juni mwaka jana.
Mke wa Rais Museveni Bi Janet Kataaha.David Muhoozi Kainerugaba.
Wakati huohuo, Luteni Kanali Don Nabaasa amepandishwa cheo na kuwa kanali kamili na akateuliwa kuwa kaimu kamanda wa SFC.
Salum Milongo/GPL
Comments are closed.