The House of Favourite Newspapers

Mwigulu Nchemba Aongoza ‘Police Family Day’

5

Timu ya polisi ikikipiga vilivyo katika timu iliyokuwa imeundwa katika kusherehekea siku hiyo.

1

Timu ikiendelea kukipiga vilivyo katika Viwanja vya Leaders Club.

2

 

3

Kamishna wa Polis Kanda Maalum Dar es Salaam, Simon Sirro akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya kundi la timu lililokuwa limeundwa kusherehekea siku hiyo.

4

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja baada ya mchezo huo kumalizika.

6

Askari polisi wanawake wakikimbiza kuku ili kumtafuta mshindi wa kuku hiyo.

7

Mshindi akiwa na kuku wake baada ya kumkamata.

8

Upande wa wanaume askari polisi nao wakikimbiza mbuzi katika mashindano hayo.

9

Katikati ni mshindi wa mbuzi aliyefanikiwa kumkamata.

10

Waziri Nchemba akizungumza jambo kabla ya kukabidhi vyeti.

11

Akikabidhi vyeti kwa askari polisi waliofanya vizuri zaidi kwenye maeneo yao ya kazi.

12

Akiendelea kukabidhi zawadi.

13

Sajenti wa Polisi, Moses Alphonce Senyagwa akipongezwa na mwezake baada ya kukabidhiwa pikipiki kutokana na ufanisi awapo barabarani kuruhusu magari kwa haraka.

14

Mgeni rasmi wa hafla hiyo Mwigulu Nchemba (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba leo amewaongoza baadhi ya askari katika hafla fupi ya Siku ya Familia iliyofanyika katika Viwanja vya Leaders Club ambapo pia ameshiriki katika mchezo wa mpira wa miguu uliofanyika viwanjani hapo, asubuhi.

Akiwa mgeni rasmi, Waziri Nchemba pia amekabidhi vyeti na zawadi mbalimbali kwa baadhi ya askari waliofanya vizuri kazini.

Baadhi ya viongozi waandamizi wa Jeshi la Polisi Tanzania, baada ya kutoka uwanjani hapo, walielekea katika Mikoa ya Kipolisi ya Kinondoni, Temeke na Ilala ambapo walitembelea Hospitali za Mwananyamala, Amana na Temeke kushiriki kufanya usafi wa mazingira na kutoa misaada maeneo hayo.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mwigulu alisema kuwa serikali itaendelea kuwa karibu na jeshi la polisi ili kuhakikisha wanaboreshewa huduma stahiki kwani kazi wanayoifanya inahitaji kupewa motisha.

Maadhimisho hayo ya siku ya familia pia yameambatana na burudani ya ngoma za asili, kuvuta kamba, kukimbiza kuku na muziki kutoka bendi ya polisi.

Na Denis Mtima/ GPL

Comments are closed.