The House of Favourite Newspapers

Mchungaji Mwingereza alivyouawa na kuliwa nyama yake

wala-watu-3

Kabila la wala watu Fore.

KABILA LA WALA WATU-02 Tunaendelea kusimulia habari ya kweli ya watu wanaokula binadamu wenzao kama tulivyoanza kueleza wiki iliyopita. Jamii ya ukoo wa Fore au Kuru wanaoishi katika nchi ya Papua New Guinea ambayo ni visiwa tuliona kwamba wanakula nyama za watu na tukaishia pale tuliposema kuwa wanakula ubongo wa watu, endelea: wala-watu-4Watu wakiwa katika hifadhi wakiandaliwa kuliwa

Jamii hii ya kabila la Fore ambao pia walipachikwa jina la Kuru hula ubongo wa binadamu na jina hilo walipewa kutokana na kuibuka kwa ugonjwa ulioitwa kuru katika eneo lao. Katika miaka ya 1950 mpaka 1960 kulikuwa na ugonjwa huo uliokuwa ukiwaua watu wengi na dawa au kinga pekee waliyokuwa wakiiamini ilikuwa ni kula ubongo wa mmoja wa aliyefariki dunia kwa ugonjwa huo japokuwa hata ambao siyo wagonjwa nao walikuwa wakiliwa kama tutakavyoona baadaye.

Jamii ya Kuru wengine huuita Kuria au Guria wakiwa na maana ya tikisa au tetemeshi ulikuwa ni ugonjwa ambao wenyeji waliopatwa walikuwa wakitetemeka mwili na hawakupata dawa na matokeo yake mamia ya watu hao walipoteza maisha.

Kitamaduni za watu hao mtu akifa kwa ugonjwa huo ilikuwa ni lazima ubongo wake upikwe na kuliwa na ndugu wa familia yake hasa wanawake na watoto kama kinga. Kinacho-fanyika ni marehemu anapasuliwa kichwa chake na wanaume kisha kutolewa ubongo na kupikwa, ukiiva hupewa wanawake na watoto.

Watu hao wanaamini kwamba ubongo huo ukiliwa familia hiyo itaondokana na balaa ya kufiwa na mtu mwingine. Hata hivyo, ugonjwa huo hivi sasa umepungua sana kwani mwaka 1950 uliua wenyeji 200 lakini mwaka 2005 aliyekufa kwa ugonjwa huo ni mtu mmoja na sasa hakuna aliyekumbwa na kufariki dunia.

Kabila hili liliwahi kuomba radhi kwa kuwaua na kuwala nyama zao wamisionari wa Kiingereza ambao walikuwa Wazungu wa mwanzo kutembelea visiwa hivyo katika karne ya 19, hivyo hali hiyo inadhihirisha kuwa kula nyama za watu kwao ni tabia ya siku nyingi.

Wamisionari hao wanne walipofika katika visiwa hivyo walikamatwa na wakauawa kikatili kwa kuchomwa na kijiti chenye ncha kali mdomoni kwa amri ya Chifu wa Mashujaa, Taleli kisha wakakatwakatwa miili yao kisha kupikwa, nyama zao zikaliwa na wenyeji hao.

 Kuuawa na kulikuwa kwa wamisionari hao  wengine ni wa Fiji, mmoja alikuwa waziri na wengine watatu walikuwa ni walimu wakiongozwa na Mchungaji George Brown ambaye alikuwa maarufu kwa kutangaza neno la Mungu, walikuwa wanakwenda kwenye moja ya jimbo la Papua New Guinea linalojulikana kwa jina la New British kuhubiri.

Mchungaji Brown alikuwa ni mhamiaji wa New Zealand akitokea Barnard Castle, Durham, England alikozaliwa. Alihamia New Papua Guinea akiwa na mkewe kwa nia ya kuhubiri neno la Mungu na alitembelea kwenye makazi ya wala watu hao ili kuwabadilisha tabia ili wawe watu wema wacha Mungu lakini matokeo yake walimgeuka na kumla yeye na wamisionari aliokuwa nao na tangu enzi hizo, watu wanaendelea kuliwa eneo hilo.

Wiki ijayo tutaeleza kile alichokiandika Mchungaji Brown kabla ya kuuawa na nyama yake kuliwa na watu hao na hali ilivyo sasa visiwani humo.

Comments are closed.