Madaha: Mastaa Mrudi Shule!
Baby Madaha
MSANII wa muziki na filamu Bongo, Baby Madaha amewataka mastaa wenzake kurudi shule kwani kwa kipindi hiki cha ugumu wa maisha na utawala wa Rais John Magufuli wataumia bila kuwa na elimu ya kutosha.
Akipiga stori na Risasi Vibes, Baby Madaha anayeunda Kundi la Scorpion Girls akiwa na Isabela Mpanda ‘Bela’ alisema kuwa, kutokana na maisha kuwa magumu na kazi za sanaa hazilipi hasa filamu, mastaa hasa wa kike wanatakiwa kuachana na tabia za kujiuza kwa wanaume hovyo na kurudi darasani kwani elimu ndiyo itawakwamua kimaisha.
“Wakati nasoma watu walikuwa wananicheka, sasa nakula mshahara kwenye kampuni ya madini ambayo tunamiliki mimi na kaka yangu yenye matawi hapa Dar na Dubai. Sijiuzi China wala Dubai kama wasanii wengine, yaani mastaa lazima mrudi shule maana ‘vyuma’ vimekaza vibaya,” alisema Baby Madaha.
Comments are closed.