12 Wauawa Kwa Shambulio la Risasi Marekani

WATU 12 wameuawa na wengine sita kujeruhiwa katika mashambulio ya kurushiana risasi katika jumba la serikali jimboni la Virginia nchini Marekani, polisi wamesema.

 

Ripoti zinasema mshukiwa katika shambulio hilo ambapo alifyatua risasi kiholela, ni mfanyakazi wa muda mrefu katika kituo cha manispaa ya Virginia.

Mtu huyo ambaye hakutajwa jina lake,  aliuawa baada ya polisi kuwasili katika eneo hilo na kumkabili, ambapo Meya wa Virginia, Bobby Dyer,  alielezea tukio hilo kuwa baya zaidi katika historia ya mji huo.

 

Kwa mujibu wa mtandao wa Marekani wa Gun Violence Archive hili ni shambulio la 150 kufanyika nchini Marekani mwaka huu.


Loading...

Toa comment