The House of Favourite Newspapers

Tanayzer: Sitamsahau Abdul Bonge

Said Othman ‘Tanayzer’

Na MUSA MATEJA| IJUMAA WIKIENDA| OVER ZE WEEKEND

MSANII wa Bongo Fleva ambaye ni zao kutoka Kundi la Tip Top Connection, Said Othman ‘Tanayzer’ ameweka wazi kuwa haitatokea hata siku moja kumsahau muasisi wa kundi hilo, Abdul Bonge kutokana na kilichomtokea mbele yake saa chache kabla hajaaga dunia.

Akizungumza na Over Ze Weekend, Tanayzer anayebamba na Ngoma ya Guta alisema, siku hiyo ilikuwa ya kwenda kumtambulisha rasmi kwenye muziki na Abdul Bonge (marehemu) alikuwa ameshika CD mkononi lakini akaanza kujisikia vibaya. “Ikabidi amuachie CD, Idd Tale na kumwambia kuwa aendeleze harakati zangu na kwa bahati mbaya baadaye akatutoka. Ni jambo kwa kweli sitokaa nimsahau kwa kuwa alikuwa msaada mkubwa kwangu, lakini hata sasa ninafanyiwa vile alivyokuwa akitaka, “ alisema Tanayzer.

Comments are closed.