ILE bahati nasibu ya Shinda Nyumba inayoendelea kwa sasa chini ya Kampuni la Global Publishers wachapishaji wa magazeti ya Uwazi, Championi, Ijumaa, Amani na Risasi inazidi kusonga mbele ambapo watu mbalimbali wanaendelea kujitokeza na kujaza kuponi kwa wingi ili kutengeneza nafasi ya kushinda zawadi mbalimbali kila mwezi zikiwemo pikipiki na simu za kisasa na hatimaye kujishindia nyumba katika droo kubwa itakayochezeshwa baadaye mwaka huu.
Huku bahati nasibu hiyo ikiendelea kuwa gumzo kutokana na msisimko iliyonayo, leo Mr Shinda Nyumba anayesepa na kijiji kila kona anakopita alikuwa mitaa ya Keko jijini Dar alikowatembelea wasomaji na wananchi kwa jumla kwa mara nyingine.
Mbali na kumshangaa Mr Shinda Nyumba, wakazi wa maeneo hayo walijitokeza kwa wingi huku wakionyesha dhahiri kupania kujishindia nyumba pamoja na zawadi mbalimbali.
“Hii nyumba lazima niipate, nimeshiriki hii bahati nasibu toka mwakani, kiukweli nimepania sana kwa mwaka huu lazima nikate kuponi niwezavyo ili kushinda nyumba,” Vincent George mfanyabiashara katika mitaa hiyo.
Kwa upande wa mwanamama Rehema Hassan alisema kuwa bahati ya kushinda nyumba ni ya kina mama na amepania kwa mwaka huu ataibuka na nyumba hiyo huku akisisitiza ataendelea kukata kuponi bila kukoma.
“Mimi nimeamua mpaka kieleweke, kila siku nakata kuponi moja tu, najua shilingi mia tano ninayowekeza kila siku ni lazima itarudi mwishoni mwa bahati nasibu hii,” alisema Rehema.
Boniphace Ngumije/GPL
Comments are closed.