The House of Favourite Newspapers

Tajiri Aliyempa Makonda Ardhi kikaangoni

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda

Na MWANDISHI WETU| UWAZI| HABARI

DAR ES SALAAM: Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema atamchukulia hatua mfanyabiashara, Mohamed Iqbar Iqbar ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Azimio Estaste, aliyemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda eneo kwa ajili ya viwanda kwa sababu eneo hilo si lake, ni mali ya serikali.

William Lukuvi

Waziri Lukuvi aliyasema hayo jana alipozungumza na Uwazi moja kwa moja kwa njia simu na kuonesha kukerwa na hatua ya Iqbar kutoa eneo hilo huku akijua si mali yake. “Sitaki ardhi itumike kama sehemu ya wafanyabiashara kutakatishia fedha zao chafu. Lile eneo ni mali ya serikali, kulikuwa na kesi mahakamani kati ya serikali na yeye Iqbar, akashindwa na hati za hukumu anazo.

“Kwanza nashangaa sana, amempaje lile eneo Makonda wakati anazo hati za kushindwa mahakamani?” alihoji Lukuvi ambaye amefanikiwa vyema kutatua migogoro mbalimbali ya ardhi nchini. Ijumaa iliyopita, Makonda alikabidhiwa ekari 1,500 za ardhi katika eneo la Lingati Kisarawe 2,
wilayani Kigamboni kwa ajili ya kujenga viwanda vidogovidogo na vya kati.

Makonda

Tajiri aliyempa Makonda ardhi kikaangonEneo hilo litakalojulikana kama Dar es Salaam Industrial Area. Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa eneo hilo, Makonda alisema ekari hizo zitagawanywa katika makundi ya uwekezaji viwanda vidogo na vya kati, ufugaji wa mifugo ikiwemo ng’ombe na mbuzi lakini pia kilimo. Hata hivyo, Makonda alitoa angalizo kwa wale wananchi wazalendo wanaojitolea kwa ajili ya jamii kwamba, wafanye hivyo wakiwa na mikono misafi.

Comments are closed.