Queen Darleen Amfungukia Ali Kiba

Abdul ‘Queen Darleen’

Na ALLY KATALAMBULA| GAZETI LA AMANI| SHOW BIZ- XTRA

FIRST Lady wa Wasafi Classic Baby (WCB), Mwanaisha Abdul ‘Queen Darleen’ amefunguka kuwa hajawahi kumkosa (kummisi) staa mwenzake wa Bongo Fleva, Ali Kiba ambaye kitambo alikuwa mshkaji wake wa karibu.

Ali KIba na Abdul Kiba

Akipiga stori na Show Biz Xtra,Queen Darleen alisema kuwa, mara ya mwisho kuwasiliana na Kiba ni miaka mingi iliyopita na wala hashangazwi na kushtushwa na ukimya huo kwa kuwa huwa anamuona kwenye runinga akiwa fiti.

Queen Darlin na baadhi ya wanafamilia wa WCB

“Nina miaka mingi sana sijawasiliana naye wala sijammisi sababu kila siku huwa namuona kwenye runinga, bila shaka atakuwa buheri wa afya. Hata namba niliyokuwa nayo sina uhakika kama ni ileile au amebadilisha, kama bado anayo ipo siku nitamcheki ila kama amebadilisha ndiyo nitolee,’’ alisema Darleen.

Toa comment