The House of Favourite Newspapers

Sabby: Ni Urembo Sarakasi na Muziki

Sabby

Na ANDREW CARLOS| GAZETI LA IJUMAA| SHOW BIZ

HAKUNA kitu kizuri katika sanaa kama kubahatika kuwa na vipaji vingi ambavyo vinaweza kukuingizia chakula cha siku. Wapo wasanii wa Bongo Fleva wenye vipaji vya kuogelea, kucheza filamu, yoga, sarakasi n.k.

Mfano Mwanamuziki Shilole na Snura hawa wana vipaji zaidi ya kimoja ambapo kama utakumbuka wasanii wote hao wanaotamba kwenye Muziki wa Bongo Fleva walikuwa wakikubalika kwenye filamu japo kwa sasa inaonekana kama wameitupa mkono na kuelekeza nguvu nyingi kwenye muziki. Sabrina Omary maarufu kama Sabby Angel naye ni miongoni mwa wasanii wenye vipaji vingi Bongo.

Alianza kufahamika kwenye filamu na tamthiliya mbalimbali kisha kwenye Muziki wa Bongo Fleva. Lakini pia unapozungumzia warembo wanaoziweza sarakasi na yoga ni wazi jina lake litakuwepo kwenye listi.

Akizungumza na Showbiz, Sabby anayetamba na Wimbo wa Inahusu anasema kuwa, alianza kujifunza mchezo wa sarakasi na yoga tangu akiwa mdogo.

“Wengi walikuwa wakinishangaa, mama alikuwa mkali sana kila akiniona nabinuka. Baada ya kuwa naruka sarakasi mara kwa mara hasa nyakati za kwenda kuoga hatimaye nikawa bora,” anasema Sabby na kuongeza:

“Kuna kipindi nikiruka mbele ya watu wananishangaa na kuona hii ni michezo ya kiume na kwamba mrembo kama mimi hasa hapa Bongo sipaswi kuwa hivi.

Sarakasi na mchezo wa yoga kwangu nachukulia kama sehemu ya vipaji ukiondoa muziki na filamu ninavyofanya.”

Showbiz pia ilitaka kufahamu kama alishawahi kushiriki mashindano yoyote ya sarakasi na yoga hadi sasa.

“Nakumbuka nikiwa shuleni nilishawahi kushiriki mashindano ya sarakasi shule kwa shule lakini

sikufanikiwa kufika mbali,” alisema Sabby. Mbali ya yoga na sarakasi, Sabby anasema kuwa, ili kuuweka mwili wake fiti mara nyingi pia

katika mazoezi yake ya kila siku hufanya push-ups (pushapu) na kukimbia umbali mrefu. “Nafanya pia mazoezi ya pumzi kama

kukimbia ambayo kiukweli yamenijenga sana na najivunia kuwa mwanamke strong,” anamaliza Sabby.

 

Comments are closed.