The House of Favourite Newspapers

Mtaalam: Bila Kukubali Kosa, Mastaa Hawa ndo`basi Tena!

Rommy Jones

Na SIFAEL PAUL| IJUMAA WIKIENDA| OVER ZE WEEKEND

WAKATI watu mashuhuri kama wanasiasa na mastaa wakihusishwa na ishu ya madawa ya kulevya ‘unga’, mtaalam wa saikolojia ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk. Chriss Mauki amefunguka juu ya mastaa na vijana wanaotamani kuacha matumizi ya madawa hayo na ulevi wa kupindukia lakini inashindikana. 

Vanessa Mdee

Baadhi ya mastaa ambao hivi karibuni walitajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuwa wanajihusisha na biashara na matumizi ya madawa ya kulevya ni pamoja na Wema Sepetu, TID, Chid Benz, Tunda, Vanessa Mdee, Mr Blue, Recho, Babuu wa Kitaa, Rommy Jones, Petit Man, Nyandu Tozi, Masogange na wengineo.

Juu ya nini kifanyike ili kuwaokoa mastaa hao na vijana ambao ni wengi mitaani wanaotumia unga, Over Ze Weekend inakuletea mahojiano maalum na Dk. Mauki ambaye anaeleza jambo pekee la kuwaokoa mastaa hao siyo kutumia nguvu au kuwapeleka polisi bali wanahitaji kutengenezwa kisaikolojia.

Petit Man na mwanaye

CHANZO CHA KUINGIA KWENYE MADAWA YA KULEVYA

Dk. Mauki anafunguka chanzo cha mastaa hao kuingia kwenye madawa ya kulevya:

“Wasanii wengi na vijana ambao hawana majina wanaingia kwenye matumizi ya madawa ya kulevya na ulevi wa kupindukia kutokana na sababu mbalimbali. Kimsingi utafiti wetu unaonesha tatizo kubwa linakua kwa kasi ya ajabu mitaani.

“Kwanza ni matatizo ya wazazi na walezi. Malezi limekuwa ni tatizo kubwa, wazazi na walezi wa sasa hawajui maendeleo ya tabia za watoto wao, wengi wao hawana muda wa kukaa na watoto wao kujua wanawaza nini na kuwasaidia kimawazo. Debate (mijadala) kati ya mtoto na mzazi au mlezi ni muhimu mno.

“Ndoa nyingi za sasa zina stresi. Watoto wameyachukua matatizo ya ndoa za wazazi wao kama nafasi ya kujiingiza kwenye ulevi kwa sababu hakuna follow up (ufuatiliaji). Hivyo katika janga hili mzazi hakwepi lawama kama yupo hai.

Dk. Chriss Mauki

“Pili, vijana wetu hawana kazi za kufanya, muda mwingi wanautumia kukaa idle (bila kufanya kazi) vijiweni na kwenye magenge ya umri-rika yasiyowajenga. Huko ndiko wanakojifunza mambo yasiyofaa.

Matokeo yake wameathirika na ulevi kroniki wa viroba (hata kama vimepigwa marufuku watatafuta njia mbadala), madawa ya kulevya na tatizo lingine ambalo linajificha zaidi ni kujichua.

Utafiti unaonesha vijana wetu wengi ni waathirika wa kujichua (masturbation), sema tu ni jambo la siri ndiyo maana halisemwi waziwazi lakini matokeo yake yanakuja kujitokeza wanapoingia kwenye ndoa kwani malalamiko ya kutotoshelezwa yanakuwa ni mengi. “Pia ieleweke kwamba tatizo la ulevi au addiction (uraibu) wa ulevi siyo mastaa tu na vijana, pia wamo wakurugenzi, mameneja wa mabenki,
makampuni na mashirika binafsi na hata ya umma.

NINI KIFANYIKE KWA MASTAA WALIOTAJWA?

“Kwanza kabisa lazima wajikubali, wakubali makosa yao kwamba kuna mahali walikosea. Kutumia nguvu haiwezekani kuwaokoa na badala yake ndiyo itakuwa basi tena. Wataangamia.

“Kuna mfano wa mzee aliyeamua kutumia nguvu kumdhibiti mwanaye wa kiume aliyeathirika na madawa ya kulevya. Alitumia fedha nyingi kumpeleka kwenye rehab (sober house).

Kiukweli mzee yule aliamini mwanaye amebadilika baada ya muda mfupi. Akamuona amekuwa smart na anapiga suti kama watoto wengine wasio na matatizo. Lakini kwa kuwa alilazimishwa bila kuridhia mwenyewe kutoka moyoni kwamba ameathirika na kudhamiria kuacha, alijikuta akirudi kulekule kama inavyotokea kwa baadhi ya wasanii.

“Kupona na uraibu wa madawa ya kulevya, asikudanganye mtu, siyo tatizo la kupona kwa muda mfupi.

“Hatuwezi kusema msanii au kijana fulani amepona wakati bado yupo kwenye mazingira yaleyale. Anazungukwa na vijiwe vya watu walewale na anaendelea kushuhudia matatizo ya kifamilia hasa ya migogoro ya ndoa za wazazi wao au malezi dhaifu ya upande mmoja.

“Kwa hiyo tukubaliane kuwa hata kwa mtutu wa bunduki, bila kujengwa kisaikolojia na wenyewe kukubali kuwa waliteleza na wapo tayari kubadilika kwa dhati, tutakuwa tunacheza ngoma isiyoeleweka na vijana wetu watazidi kuangamia.

“Uwepo wa nyumba za kuwasaidia ni sahihi kabisa na ziongezewe nguvu lakini je, mazingira ya nyumba hizo yanawabadili au huko ndiko wanakutana na wenzao watakaowaharibu zaidi wanaporudi mitaani na kujikuta wamekuwa na network kubwa zaidi? Tujitafakari, vijana wetu wanaangamia

SHINDA NYUMBA AWAMU YA PILI YATIKISA JIJI LA DAR ES SALAAM

Comments are closed.