The House of Favourite Newspapers

Wewe si Mjamzito Lakini Unakosa Hedhi, Unaijua Sababu?-2

WIKI iliyopita tuliishia kuangalia jinsi ukosefu au upungufu wa homoni zinazochochea kukua na kufanya kazi kwa via vya uzazi kunavyoweza kukuathiri, ugonjwa ambao kitaalamu hujulikana kama Kallmann Syndrome.

Matatizo katika tezi ya Pituitary:

Vyanzo vinavyohusisha tezi ya pituitary ni pamoja na kuwepo kwa kiwango kikubwa cha homoni ya Prolactin katika damu au kwa kitaalamu huitwa Prolactinemia. Prolactin ni homoni inayochochea uzalishaji wa maziwa wakati wa kunyonyesha.

Hali ya kuwa na Prolactin nyingi katika damu inaweza kutokea iwapo kuna uvimbe unaoitwa Prolactinoma katika tezi ya Pituitary.

Kuwepo kwa uvimbe mwingine wowote katika tezi ya Pituitary: Pituitary hushindwa kufanya kazi baada ya seli zake kufa, hususan iwapo mama alipoteza damu nyingi wakati wa kujifungua.

Kuharibika kwa tezi ya Pituitary baada ya seli zake kushambuliwa na mfumo wa kinga ya mwili. Kuwa na historia ya kupata tiba ya mionzi inayohusisha tezi ya pituitary.

Matatizo katika ovary:

Vyanzo vinavyohusisha matatizo katika viwanda vya kuzalisha mayai ya kike, yaani Ovaries ni pamoja na kutozalishwa kabisa kwa mayai Anovulation. Kuwepo kwa kiwango kingi cha homoni za kiume katika damu (hyperandrogenemia).

Ovary kuwa na vifukovifuko (polycystic ovarian syndrome) na kushindwa kufanya kazi zake vizuri. Haya ni matatizo ya homoni ambayo huwapata baadhi ya wanawake walio katika umri wa kuzaa. Kufa na kushindwa kufanya kazi kwa Ovary kabla ya muda wake.

Ugonjwa wa kuzaliwa unaoitwa Turner syndrome ambao huambatana na kukosekana kwa ovary au ovary kuwa changa kuliko kawaida, msichana kushindwa kuvunja ungo na msichana kuwa na kimo kifupi kuliko kawaida.

Ugonjwa huu hutokana na matatizo ya kijenitikia Genetic Disease.

Ukosefu wa kimaumbile wa Ovary ambao hutokea wakati wa ukuaji. Kufa kwa ovary baada ya seli zake kushambuliwa na mfumo wa kinga ya mwili. Historia ya kuwahi kupata tiba ya mionzi au madawa yanaathiri Ovary.

Ugonjwa wa kurithi wa Galactosemia unaoambatana na kuwa na kiwango cha juu cha sukari aina ya Galactose katika damu. Matatizo ya kimaumbile katika njia ya mfumo wa uzazi wa mwanamke yanayoweza kusababisha na ukosefu wa hedhi ni pamoja na…

Comments are closed.