The House of Favourite Newspapers

Amber Lulu: Haikuwa Rahisi Kuwa na Country Boy

Lulu Auggen ‘Amber Lulu’

Na ANDREW CARLOS| GAZETI LA IJUMAA| SHOW BIZ

MUUZA nyago ambaye ameingia rasmi kwenye Muziki wa Bongo Fleva   , Lulu Auggen ‘Amber Lulu’ amesema kuwa haikuwa jambo rahisi kumuweka staa wa Hip Hop, Ibrahim Ayoub Mandingo ‘Country Boy’ katika rada zake na kufanikiwa kutoa naye ngoma.

Country Boy

Amber Lulu aliiambia Showbiz kuwa, anafarijika kusikia ngoma yake ya Watakoma aliyoshirikiana na Country Boy ni miongoni mwa ngoma inayopendwa kila kona lakini kuna mengi watu hawajui.

Amber Lulu’

“Nashukuru Mungu kwa kuwa ndo kwanza nimeingia kwenye muziki na Wimbo wa Watakoma, lakini nikwambie tu haikuwa jambo rahisi kumshawishi Country Boy kukubaliana na mimi kwa kuwa ndo kwanza nilikuwa naanza muziki. Bahati nzuri ni muelewa, alinisikia mara nyingi kisha akanikubalia hadi kuingia studio na kuibuka na wimbo huo,” alisema Amber.

 

Comments are closed.