The House of Favourite Newspapers

Wanene Entertainment Presents: Chin Bees ‘Pepeta’ – (Official Music Video)

Baada ya kuachia audio ya wimbo wake mpya ‘Pepeta’, rapper kutoka Tanzania Chin Bees ameiachia official music video ya wimbo huo.

Chin Bees ambaye sasa yupo chini ya uongozi wa Wanene Entertainment, amerudi tofauti kwenye playlists za bongo fleva na wimbo wa ‘Pepeta’ ambayo miondoko yake inafanana na style ya muziki wa Trap Music ambao wengi wetu tunausikia sana ukiimbwa na wasanii wa Marekani kama Migos na wengine.

Nataka kuwa mtu wa kutofanya style moja, mimi nataka niwe nafanya style tofauti na kila moja niifanye kwa ubora mzuri. Video ya Pepeta imefanyika chini ya director Rahul, lights na shots zile amefanya mtu mmoja anaitwa Aanand Lonkar… Pepeta sio trap ambazo tunazisikia kwenye game, ni trap tofauti, kuanzia video, mastering ya audio, zote ziko perfect.” – Chin Bees ameiambia Bongo5

Wimbo huu umetayarishwa na Mmarekani aitwaye Thomas Crager na huku mastering ikifanyika katika studio za Wanene na sound engineer wao Sarthak ikiwa pia ni project ya kwanza ya muziki ya lebo kubwa nchini Wanene Entertainment.

Itazame video ya Chin Bees ‘Pepeta’ hapa chini.

IMEANDIKWA NA: Sandra Brown.

Subscribe kwenye YouTube Chanel yetu ya Global TV Online ili zote kali zinazotufikia iwe ni siasa, michezo, comedy, burudani, stori za mastaamuziki na nyingine zikufikie kwa wakati.

Comments are closed.