The House of Favourite Newspapers

Mmeachana, Sasa ya Nini Kuombeana Mabaya?

Na GABRIEL NG`OSHA| IJUMAA WIKIENDA| XXLOVE

NIANZE kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa rehema, fadhila na upendo wake wa ajabu kwangu na kwako, anaendelea kutufanya wapya kila siku, tumuombe atuongezee maarifa zaidi. Kwa upande wangu namuomba anipe nyenzo mpya kila siku kwa ajili ya kuisaidia jamii yangu kupata elimu sahihi ya uhusiano na maisha kwa jumla.

Niwapongeze wanawake wote duniani kwa kusherekea Siku ya Wanawake Duniani wiki iliyopita. Jambo moja la kuwakumbusha na kuwashauri ni kuwaheshimu waume zenu siku zote bila haki husika kuingilia ndoa zenu. Mada ya wiki hii inazungumzia baadhi ya wapenzi kuombeana mabaya baada ya kuachana au penzi lao kwisha, hii si sawa hata kidogo.

Kimsingi nakushangaa mwanaume ambaye umeachwa na mpenzi wako kisha unamsemea maneno mabaya kana kwamba hamjawahi kuwa wapenzi, wachumba au wanandoa.

Nazidi kukushangaa hasa pale unapomuombea mwenza wako apatwe na mabaya kwa sababu aliachana na wewe au mliachana. Inashangaza unapojiaminisha mbele ya marafiki zako kuwa mwenza wako hawezi kuishi bila wewe kwa sababu alikuwa anakutegemea kwa kila kitu. Wenye busara wanasema kuwa mwanamke Sidhani kama ni sahihi, sina uhakika kama mlipendana na kuamua kuwa wapenzi ili baadaye…

Unayemsema vibaya mumeo au mpenzi wako mbele ya mashoga zako kwa sababu mmeachana au amekuacha, huo ni ulimbukeni. Utafiti wangu unaonesha kuwa sehemu kubwa ya wapenzi wanapoachana, wamekuwa wakiombeana mabaya, kama mwanamke ametoka kwa mwanaume mwenye fedha basi mwanaume anatamani mwenza wake apate majanga ili tu ajutie kuachana kwao na wakati mwingine amkumbuke yeye.

Ndugu yangu maisha hayaendi hivyo, kama mmeachana ni vyema mkabaki kuwa marafiki, haijalishi mmeachana kwa mtindo gani, mnaweza kuwa hamsemeshani lakini si kwa kumnuia mwenzio mabaya.

Sidhani kama ni sahihi, sina uhakika kama mlipendana na kuamua kuwa wapenzi ili baadaye mje mnuniane, mchukiane na muombeane mabaya. Hiyo ni roho mbaya ya kishetani. Hata hivyo, huna mamlaka ya kufanya kile unachokifikiria kwa sababu riziki yake na yako zote zinatolewa na maulana.

Unapomuwazia mwenzio mabaya, ujue hata wewe unajifungia riziki zako.

Hivi mapenzi ni vita? Ni uhasama?

Kama imetokea mmeshindwana tabia na kila mtu akaamua kuanzisha maisha yake mengine nje ya wewe, kuna tatizo gani? Pengine mmesuluhishwa, mmeshauriwa sana lakini mwisho wa siku imeshindikana na ulivyo huna aibu, wewe mwenyewe ndiye chanzo cha kuvunjika kwa uhusiano wenu, wewe ndiye hasa uliyesababisha mchumba, mkeo au mumeo kukukimbia.

Leo unamuombea mabaya! Hivi ikitokea ukapata mwenza mwingine na mwingine na mwingine tena, wote mkaachana au wakakuacha, wote utawaombea mabaya?

Unadhani kati yako na yeye nani atakuwa na tatizo?  Kwa mtu anayejua kujitathmini kwa maana ya kujirekebisha, kuachwa na wapenzi kadhaa, wewe ndiye mwenye tatizo na si wao kama udhaniavyo.

Fanya marekebisho katika mtazamo wako wa kufikiri juu ya yule ambaye mmeachana au amekuacha. Muombee baraka na maisha mema huko aliko kisha mwambie Mungu:

“Kama f’lani ulipanga awe mchumba, mke au mume wangu, naamini ipo siku atakuwa tu hata kama itakuwa ni kwa mapito ya miaka kadhaa.” Mpenzi msomaji kwa ushauri na maoni, tembelea ukurasa wetu wa Gazeti la Ijumaa Wikienda, Insta:@mimi_na_uhusiano au jiunge na M&U WhatsApp kwa namba 0679 979 785.

Comments are closed.