The House of Favourite Newspapers

#GlobalCelebrities: DJ Black Coffee Wa South Africa Kushirikishwa Kwenye Mixtape Mpya Ya Drake ‘More Life’

Baada ya kushinda tuzo ya BET ya Best International Act: Africa mwaka 2016, DJ maarufu kutoka South Africa DJ Black Coffee aliendelea kupasua anga kulitafuta soko la muziki la Marekani na kurekodi nyimbo na baadhi ya majina makubwa kwenye game ikiwemo Alicia Keys na P Diddy mpaka kufikia kulipata dili hili…

Hivi karibuni kulikuwa na tetesi za kuwa DJ Black Coffee yupo mazungumzoni na management ya Drake kuona uwezekano wa wawili hao kushirikiana kwenye mixtape mpya  ‘More Life’ ya rapper huyo.

Mara ya mwisho Drake kushirikiana na msanii wa Africa (Wizkid) tulishuhudia kazi hiyo (One Dance) ikitengeneza historia na kuwa moja ya ngoma kali za mwaka sio tu kwa Africa bali kwa dunia nzima, na sasa bahati aliyoipata DJ Black Coffee kushirikiana na msanii huyo kwenye project hiyo mpya inaleta mategemeao mengine makubwa zaidi kwa wadau wa muziki Africa.

Kwa sasa bado haijajulikana DJ Black Coffee atafanya nyimbo ngapi kwenye mixtape mpya ya rappa Drake ila kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na MTV Base tutegemee kusikia mifinyo ya DJ huyo kwenye ‘More Life’ mixtape mpya ya Drake.

Je, wewe unaonaje? DJ Black Coffee ataweza kumfunika Wizkid na ‘One Dance’ kwenye hii project mpya? Tubonge kwenye comments.
Imeandikwa Na: Sandra Brown.
Subscribe kwenye YouTube Chanel yetu ya Global TV Online ili zote kali zinazotufikia iwe ni siasa, michezo, comedy, burudani, stori za mastaamuziki na nyingine zikufikie kwa wakati.

Comments are closed.