The House of Favourite Newspapers

New Music: Bank W Amekuja Na Hii Mpya ‘Blessing Me’. Itazame Hapa – (Video)

Msanii wa muziki kutoka Nigeria Banky W ameachia wimbo wake wa kwanza kwa mwaka 2017, na ujumbe wake unaweza kukutia moyo na wewe ambaye kwenye maisha unapitia changamoto nyingi.

Banky W anaisogeza kwetu video ya wimbo wake wa kwanza ‘Blessing Me’ kwa mwaka 2017, na kwa mujibu wa staa huyo wa muziki wa R&B, ameamua kuachia wimbo huu kama wimbo wake wa kwanza kwa kusudi kabisa ikiwa kama ni nafasi yake ya kumshukuru Mungu kwa kuendelea kumbariki katika kutafuta kwake na pia kumshukuru Mungu kwa kumnusuru na ajali ya kuungua moto wiki chache zilizopita.

Kupitia Instagram page yake, Banky W ameandika:

”  Kama mnavyojua, wiki iliyopita nyumba yangu ilishika moto hali iliyokuwa ya kutisha kwa wakati huo. Lakini badala ya kusononoeka na baadhi ya mali nilizopoteza nimeamua kumwimbia Mungu wangu kwa sifa na shukrani kwa kuwa ameyakomboa masiha yangu. Nasherekea maisha na nitazidi kuzihesabu baraka zote zinazoendelea kunishukia… kwa changamoto nazopitia nina uhakika wa kuwa mwisho wa siku nitasimama kwa ushujaa mbele za Mungu wangu. Kwahiyo wimbo huu ni kwa ajili ya mtu yeyote anayepitia kipindi kigumu sasa hivi, lakini pia wimbo huu ni kwa ajili ya wale wote walioweza kupambana na changamoto hizo na kuibuka mashujaa mwisho wa siku.

Naamini kuwa kitendo cha kumsifu na kumshukuru Mungu kwa baraka zote maishani mwako hufungua milango ya baraka nyingi zaidi. Hivyo kwenye video hii utaniona nikiinuliwa kutoka kwenye maisha ya asiyekuwa nacho mpaka kwenye maisha mtu mwenye nacho. Utaona pia kila kitu kuhusu maisha yangu kikibadilika nikiendelea kumsifu na kumshukuru Mungu. Mwisho wa video hii utakuwa umeweza kuiona story yangu nzima ambayo pengine inaweza ikawa stori ya mtu mwengine…. ” – Banky W

Itazame video hiyo hapa chini.

 

Imeandikwa Na: Sandra Brown.

Subscribe kwenye YouTube Chanel yetu ya Global TV Online ili zote kali zinazotufikia iwe ni siasa, michezo, comedy, burudani, stori za mastaamuziki na nyingine zikufikie kwa wakati.

 

Comments are closed.