The House of Favourite Newspapers

Habari Njema kwa Watumiaji wa Smartphone Tanzania

KAMPUNI  ya simu ya Tecno Mobile ina taarifa njema kwa watumiaji wa simu bora nchini  Tanzania ambapo inatarajia kuingiza sokoni simu mpya ya TECNO L9 Plus sokoni, hivyo imetoa nafasi ya upendeleo kwa wapenzi wa simu hizo kuweka oda mapema ili waipate kabla ya wateja wengine madukani.

Simu ya TECNO L9 Plus inasifika kwa kuwa na uwezo mkubwa wa betri inayoweza kukaa na chaji hadi saa sabini na mbili bila kuishiwa nguvu.  Betri ya simu hii ni 5000 mAh, lakini pia simu hii inakuja ikiwa na aina mpya ya usalama kwani imewekewa usalama wa alama ya vidole. TECNOL9 Plus ina kamera yenye megapixel 13 kwa nyuma na 5 kwa kamera ya mbele huku ikiwa na kioo kikubwa cha  inchi 6  kinachomwezesha mtumiaji kuangalia video vizuri,

Kitu cha kustaajabisha kuhusu TECNO L9 plus  ni kuwa simu hii inapoisha chaji  mtumiaji anaweza kuichaji kwa muda  wa dakika tano  (5) tu  na akaweza kupiga picha zaidi ya elfu moja (1000)  Ina uwezo wa kuchaji haraka zaidi na kuokoa muda wa mtumiaji  kuisubiri simu wakati kuna mambo mengine anataka  kufanya.

Wateja wanatakiwa kuweka oda mapema ili waweze kuipata simu hii  na zawadi zenye thamani ya laki moja kutoka kampuni ya Tecno Mobile.  Mteja anatakiwa kulipa kiasi cha shilingi 30,000 tu, atakuwa ameweza kuingia katika orodha ya kupata zawadi hizo ambazo ni headphone maarufu za Boom na Begi la mgongoni.  Zawadi hizi ni kwa wateja walioweka oda na wataweza kuzichukua siku watakayokuwa wanakabidhiwa simu zao mara tu zitakapofika Tanzania katikati ya mwezi wa tatu (Machi).

Kampuni ya Tecno Tanzania imepanga tarehe 21 mwezi wa tatu kuwa ndio siku wateja walioweka oda ya TECNO L9 plus watakabidhiwa simu  zao eneo la City Mall,  Dar es Salaam, iliyopo makutano ya Barabara za Bibi Titi na Morogoro muda wa saa tisa alasiri.

Wateja na wapenzi wa simu za Tecno watatakiwa kuweka oda zao katika maduka yafuatayo yanayopatikana jijini Dar es salaam, kuanzia tarehe 10 Machi mpaka tarehe 20 Machi 2017

Maduka  na meneo yanakopatikana ambapo wateja  wanaweza kuweka oda mapema.   

 

 

1 TECNO Exclusive Mobimart  Dar Shop  Kariakoo
2 TECNO exclusive Mobile Plaza Dar shop Kariakoo,

Uhuru Street

3 Freedom 4 Kariakoo, Msimbazi Road
4 TECNO exclusive City Mall Dar Shop Posta, kona ya Bibi Titi na Morogoro Road.
5 Jumbo Creation LTD Posta
6 RAM 3 Kariakoo
7 Electro Point Posta, Samora Street
8 Philipino Posta , Clock Tower
9 Freedom Electronics 1 Posta, opposite JM Mall
10 SAPNA 1 Posta , Samora Street
11 Phone 1 Mlimani A Mlimani City Mall

 

Comments are closed.