Miss Tanzania Aja na Somo la Urembo

Nafue Nyange anayefahamika zaidi Kama GlamMadam (kulia), naye akijaribu kufafanulia zaidi waandishi wa habari namna ishu hiyo itakavyokuwa

NARGIS Mohammed ambaye alikuwa mshindi wa tatu katika Shindano la Miss Tanzania msimu wa 2003/04, ameamua kuja kivingine baada ya kuanzisha somo la urembo.

Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatili uzinduzi huo.

  Nargis ambaye anashirikiana na Nafue Nyange anayefahamika zaidi Kama GlamMadam, wameamua kufanya hivyo kwa ajili ya wanawake na vijana ambao wangependa kujifunza fani ya urembo.

Miss Tanzania 2003/04, Nargis Mohammed akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo.

Akizungumza na waandishi wa habari Masaki jijini Dar es Salaam mapema leo, Nargis alisema: “Mafunzo haya hayachagui jinsia kwani nia yetu kubwa ni kuwawezesha wenzetu na kuwapa ujuzi ili waweze kujiinua kiuchumi kama wajasiriamali na kujijenga kimaisha na kujikwamua kutoka kwenye umaskini.”

Nargis aliendelea kwa kusema mafunzo hayo yatatolewa kwa bei nafuu kupitia tovuti yao ya www.glammadamlive.com ambapo kujisajili unatakiwa kulipia ada Sh 10,000 za Kitanzania kupitia mitandao ya simu ya M-Pesa na Tigo Pesa na kwa wale walio nje ya Tanzania wataweza kutumia VISA, MasterCard, American Express na kadhalika. Malipo hayo ni ya mwezi mmoja.

HABARI/PICHA: MUSA MATEJA/GPL


Loading...

Toa comment