The House of Favourite Newspapers

Nyota Dzeko Ndiye Mfalme wa Roma

Dzeko.

BAADA ya kufanya vibaya msimu uliopita ambao alifunga mabao kumi tu, hakika msimu huu staa huyo amerejea kwa kasi ya hali waliokuwa kwenye kikosi cha Wolfsburg ambacho kilitwaa ubingwa wa Ujerumani, Bundesliga.

Msimu huo staa huyo alifanikiwa kufunga mabao 36, lakini misimu iliyofuata hakuweza kufanya tena vizuri kwa kiwango hicho.

Hata hivyo, mshambuliaji huyo kwa sasa anawafunga mdomo baadhi ya mashabiki wa Roma ambao msimu uliopita walikuwa wakiupigia kelele uongozi wa timu hiyo kuwa ulipoteza fedha bure kumsajili mchezaji huyo. Lakini kiwango alichokionyesha msimu huu cha kufunga mabao nane kwenye michezo nane ya Ligi ya Europa, ni sahihi kuwa huyu alikuwa mchezaji sahihi wa kusajiliwa na timu hiyo inayoshika nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu ya Italia.

“Maisha ya Manchester City hayakuwa mazuri kwangu, labda naweza kusema kuwa hapakuwa sehemu sahihi kwangu kwa wakati ule, lakini sasa nafurahia kiwango changu naona kuwa nitaweza kufanya vizuri zaidi siku kadhaa mbele,” alisema mshambuliaji huyo mwenye uwezo wa juu wa kupachika mabao.

Hadi sasa tayari mshambuliaji huyo ameshaweka rekodi ya kuwa mchezaji wa tatu kwa Roma kufi kisha mabao 30 kwa msimu mmoja. Endapo Dzeko alifunga mabao manne kwa sasa atakuwa ndiye mshambuliaji ambaye amefunga mabao mengi zaidi kwa msimu mmoja kwenye timu hiyo.

“Nilipokuwa City tulifanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England baada ya kupita miaka 44, naamini hata hapa Roma kuna siku tutafanya maajabu,” alisema staa huyo ambaye timu yake ipo nafasi ya pili kwenye ligi wakiachwa pointi nane na vinara Juventus.

Mshambuliaji huyo ambaye ameshacheza michezo 510 na kufunga mabao 222, alipata mafanikio makubwa zaidi alipokuwa kwenye kikosi cha Wolfsburg ambacho alikichezea michezo 142 na kufunga mabao 85. Kwenye timu yake ya taifa, Dzeko ameichezea michezo 82 na kufunga mabao 49.

Comments are closed.