The House of Favourite Newspapers

Kutoka na Damu Ukeni ‘Uterine Bleeding’

HILI ni tatizo linalomtokea mwanamke aliye katika umri wa kuzaa, ni tatizo ambalo husababisha damu itoke ndani ya kizazi kupitia ukeni.

Ni hali itokanayo na mabadiliko ya kawaida ya mifumo ya mwili. Hali  hii  inaweza  kutokea  katika mzunguko wa kawaida wa hedhi na wapo wanawake wengine huwatokea  kwa  kiasi kidogo wanapokuwa  katika siku za upevushaji  mayai.

Hali ambayo siyo ya kawaida ya kutokwa damu ukeni ni pale damu ya hedhi inapotoka  nyingi na kwa muda mrefu au damu inaweza kutoka nyingi kwa kufuata siku za hedhi na kwa muda wa zaidi ya siku saba au ikatoka katika siku ambazo siyo za hedhi.

Mfano,  umeshamaliza  kubleed,  unapumzika  siku  kadhaa  halafu  unaanza  tena,  hili  pia ni tatizo kubwa  na halihusiani na mzunguko  wa hedhi.

CHANZO CHA TATIZO NA UCHUNGUZI

Vipo vyanzo kadhaa vya tatizo hili ambavyo vinahitaji uchunguzi wa kina. Tutaanza kuvielezea kwa undani ili kama upo katika mojawapo ya makundi hayo uweze kuchukua hatua mapema.

Kwanza ni tatizo la kutokwa na damu ukeni wakati wa ujauzito. Mwanamke mjamzito hategemei awe anatokwa na damu ukeni, endapo itakuwa hivyo basi chanzo kinaweza kuwa kuharibika kwa mimba, mimba kutungwa nje ya kizazi hasa kwenye mrija wa mayai, damu kutoka katika kondo la nyuma, mabaki ya mimba iliyoharibika na matatizo mengine ya kizazi ambayo kitaalamu wanawake wenye umri wa miaka 40 au ambao wana historia ya maambukizi sugu ya  mdomo wa kizazi.

Tatizo hili huonekana kwa kuchunguza mdomo wa kizazi. Hizi polyps au vinyama ni vema vichunguzwe kwa umakini kwani wakati mwingine vinaweza kuwa ni kansa. Uchunguzi wa kina utafanyika katika kliniki za madaktari bingwa wa magonjwa ya kinamama.

Nne ni kasoro za kizazi. Hapa kizazi kinaweza kuwa kimekaa vibaya au hakijarudi vizuri baada ya kujifungua  na ukajikuta damu inaendelea tu kutoka kwa miezi kadhaa, kulika kwa mlango wa kizazi na kuvimba kwa tabaka la ndani la kizazi, maambukizi sugu ya kizazi, vyote huchunguzwa kitaalam na vipimo  na utaratibu wa tiba utapangwa na daktari bingwa wa akina mama.

Tatizo la tano tunaita  ‘endometriosis’. Hii ni hali ambayo tabaka la ndani la kizazi linakuwa nje ya kizazi na humfanya mwanamke apatwe na mauvivu makali ya chini ya tumbo na kiuno chote huku akiwa anatokwa na damu kidogokidogo ukeni ingawa wakati mwingine huwa nyingi.

Hali hii husababisha ugumba, mwanamke hulalamika maumivu wakati wa tendo la ndoa na kuhisi uzito upande wa chini huku akipata shida wakati wa kukojoa na haja kubwa. Tatizo la sita ni magonjwa sugu mwilini mwa mwanamke kama tatizo la damu kuganda, shinikizo la juu  la damu, matatizo ya moyo, uwepo wa sumu mwilini kutokana na mazingira ya kazi au unywaji wa pombe kupita kiasi, magonjwa ya ini, ukosefu au upungufu wa vitamin B.

Kwa ujumla uchunguzi hutegemea na historia  ya ugonjwa na daktari atakavyoona vinafaa. Tatizo hili pia linaweza kuwatokea watoto  ambao hawajavunja ungo, hivyo linapotokea ni vema uchunguzi wa kina ufanyike.

Saba ni tatizo linalohusiana na mfumo wa homoni mwilini, hapa mgonjwa atalalamika siku zake zinaenda bila ya mpangilio, hapati mimba na wala hajui tarehe zake za kuingia kwenye hedhi.

Upevushaji wa mayai haupo na hana historia ya kutumia njia ya kuzuia mimba kwa madawa. Katika kundi hili pia mimba kwa kutumia sindano au vipandikizi na sasa wanapata siku zao bila mpangilio.

Hawa tatizo kubwa linakuwa katika mfumo wa homoni au vichocheo na wanahitaji uchunguzi wa kina kwa madaktari bingwa wa matatizo ya uzazi katika hospitali za mikoa.

NINI CHA KUFANYA?

Endapo unashabihiana na mojawapo ya makundi hapo juu, basi unashauriwa uwaone madaktari katika hospitali za mikoa au wilaya kwa uchunguzi wa kina.

Tumeona baadhi ya sababu mbalimbali, basi usichelewe ili tatizo lisije kufikia mahali ambapo gharama za kutibu zitakuwa kubwa, muda utakuwa mrefu au lisitibike kabisa.

Comments are closed.