Khadija Kopa, Msagasumu, Harmorapa, Nature jukwaa moja Pasaka Dar Live

Harmorapa na aliyekuwa mpenzi wake.

KONGWE kwenye gemu ya Bongo Fleva, Juma Kassim Ally ‘Nature’ anatarajiwa kumpandisha kwa mara ya kwanza jukwaani msanii ambaye ni gumzo jijini, Athuman Omary ‘Harmorapa’ katika Sikukuu ya Pasaka ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo MbagalaZakhem jijini Dar.

Juma Nature.

Akizungumzia shoo hiyo, Mratibu na Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo alisema kuwa usiku huo, mashabiki wote wa Nature na Harmorapa wajitokeze kwa wingi kwani mbali na kuimba pamoja Wimbo wa Kiboko ya Mabishoo, watawarusha kwa wimbo mpya ambao ni sapraizi.

Khadija Kopa.

“Wengi wamezoea kumuona Harmorapa mitandaoni na kwenye magazeti pia kumsikia redioni na kwenye TV lakini hawajawahi kuona shoo yake ipoje, sasa mwambie na mwenzako kwa mara ya kwanza Harmorapa kipenzi cha wengi atashuka jukwaani na mastaa kibao tofauti na Nature na kufanya shoo ambayo haijawahi kutokea Dar Live,” alisema Mbizo.

Msaga Sumu.

Mbizo aliongeza kuwa, mbali na uwepo wa Nature na Harmorapa, jukwaa litavamiwa pia na Malkia wa Mipasho, Khadija Kopa akiwa na kundi zima la T.O.T Taarab, Dulla Makabila, Msaga Sumu pamoja na pambano la ngumi.

“Mapema kuanzia asubuhi kutakuwa na Makhirikhiri wa Tanzania ambapo watoto wote kwa pamoja watapata kujiachia kwa michezo ya kuogelea, kucheza kwenye treni na kwenye ndege na mashindano mbalimbali,” alisema Mbizo.
Toa comment