The House of Favourite Newspapers

Mr Shinda Ndani ya Temeke na Kijichi Tena

Jimmy akimsaidia kujaza kuponi Shamila Hemed mkazi wa Kijichi.

BAHATI na Sibu ya Shinda nyumba inayoendelea kwa sasa chini ya Kampuni la Global Publishers wachapishaji wa magazeti ya Uwazi, Championi, Ijumaa, Amani na Risasi inazidi kusonga mbele ambapo watu mbalimbali wanaendelea kujitokeza na kujaza kuponi kwa wingi ili kutengeneza nafasi ya kushinda zawadi mbalimbali kila mwezi zikiwemo pikipiki na simu za kisasa  hatimaye kujishindia nyumba katika druo kubwa itakayochezeshwa hapo baadaye.

Jimmy akimsaidia kujaza kuponi Shamila Hemed mkazi wa Kijichi.

Huku bahati na sibu hiyo ikiendelea kuwa gumzo kutokana na msisimko iliyonayo wakati huu, leo yule Mr Shinda Nyumba anayesepa na kijiji kila kona anakopita kwa mara nyingine alikuwa katika mitaa ya  Temeke na Kijichi na kuzidi kuwapagawisha watu kutokana na urefu wake pamoja na namna ya kipekee anavyoitangaza promosheni ya Shinda Nyumba.

Shinda Nyumba na Jimmy wakiwa katika picha ya pamoja na wasomaji wa magazeti ya Global kutoka Kijichi.

Mbali na kumshangaa Mr Shinda Nyumba na timu yake wakazi wa maeneo hayo walijitokeza kwa wingi huku wakionyesha dhahiri kupania kujishindia nyumba pamoja na zawadi mbalimbali kwa kununua magazeti kwa wingi pamoja na kujaza kuponi.

Shinda Nyumba akimsaidia kujaza kuponi msomaji wa magazeti ya Global.

 

Jimmy akimsaidia kujaza kuponi ya Shinda Nyumba, Angela Mushi, mkazi wa Kijichi.
Afisa Usambazaji wa Global, Jimmy Harooub akimpa maelekezo ya kujaza kuponi Subira Zamwe, mkazi wa Temeke.
Msomaji wa magazeti ya Global, Fatuma Jaffari akijaza kuponi ya Shinda Nyumba.
Mr Shinda Nyumba akiwa katika picha ya pamoja na wasomaji wa magazeti ya Global Publishers maeneo ya Temeke.
Mr Shinda Nyumba akimsaidia kujaza kuponi Nasra Mustapha, mkazi wa Temeke baada ya kununua Gazeti la Ijumaa Wikenda.

PICHA: BONIPHACE NGUMIJE

Comments are closed.