The House of Favourite Newspapers

Kabila la Wala Watu-13, Wenyeji Hupata Mlo Mara Mbili kwa Siku, Chai ya Mchaichai…

NA ELVAN STAMBULI NA MTANDAO| GAZETI LA UWAZI| MAKALA

NAENDELEA kusimulia jamii inayokula nyama ya watu inayoishi Papua New Guinea; endelea. Nielezee kidogo kuhusu nchi hiyo ambayo ni kisiwa.

Sensa ya mwaka 1990 inaonesha kuwa nchini Papua New Guinea kuna watu 3,761,954  na mji mkuu wao unaitwa Port Moresby  ambao una wakazi 220,000, miji mingine na idadi ya watu katika mabano ni  Lae (90,000),  Madang (30,000),  Mt Hagen (45,000), Wewak (23,000) na Goroka (25,000).

Licha ya yale makabila mawili yanayojulikana kwa kula nyama za watu, Wakorowai  na Wafure, kuna makabila mengine mengi katika kisiwa hicho. Lakini lugha inayozungumzwa na watu wengi inaitwa Tok Pisin (talk pidgin), hata hivyo,  baadhi yashule hufundisha kwa lugha ya Kiingereza kwa msaada wa wamisionari licha ya wengi wao wa kwanza kuingia katika kisiwa hicho kuuawa na miili yao kuliwa, hivi sasa dini ya Kikristo imeanza kusambaa baada ya jitihada kubwa ya kuelimisha hasa wale wanaokula nyama za watu.

Siyo Wamisionari tu, hata watalii na wana habari kadhaa waliokuwa na shauku ya kujua kwa undani makabila yanayokula watu, baadhi yao waliishia kuliwa nyama zao na  sehemu zao za siri kupikwa na vidole kufanywa supu ya ‘mashujaa’ waliowaua na kuwakatakata vipande.

Kabla ya kuingia Wazungu watafiti na Wamisionari, makabila ya huko yalikuwa maadui, kwamba kabila fulani likienda kwenye eneo la kabila lingine, basi kurudi salama ilikuwa ni nadra kwani waliuana na miili yao kuliwa.

Kwa kawaida katika kisiwa hicho wavulana wanapokuwa wamefikia umri wa kubalehe,hujenga nyumba zao na kulala humo na kuachana na wazazi wao.Wanapooa hutozwa mahari, mara nyingi ni ya wanyama hasa nguruwe na siku ya kufungishwa ndoa za kimila huandaliwa kinywaji maalum na sherehe kubwa hufanyika.

Wenyeji wengi wana afya nzuri kutokana na kula vyakula vya asili kama vile magimbi, viazi vitamu, matunda ya porini, mchele, samaki wanaovuliwa baharini na kwenye mito, wanyama wa porini, nyama ya nguruwe, kuku na ndege wa aina mbalimbali kama vile bata mzinga au kanga (cassowaries ), huku wakitumia tui la nazi au mafuta ya nguruwe. Wananchi wa visiwa hivyo hufuga na kula nguruwe, kuku, bata, lakini hula pia nguchiro, kasa, aina fulani ya funza wanaowapata kwenye magogo na panya.

Wanalima miwa, mpunga, embe, nazi, viazi na magimbi. Watu wa Papua New Guinea wana desturi ya kufanya sherehe za kimila kila mwaka ambapo watu hujipamba kwa kujipaka rangi kwenye nyuso zao kwa umaridadi mkubwa, wengine huchukua hata watoto wao na wanaume huwa na mikuki na kuimba huku wakicheza na kufurahi na katika shughuli hiyo nguruwe wengi huokwa na kuliwa nyama yao baada ya kupakwa chumvi ya asili ambayo hupatikana kwa kuchemsha maji ya bahari. Watu wa huko huwa wanakuwa na mashindano ya kushindania vitu mbalimbali kama vile nani amevuna zaidi mazao msimu huo, mashindano ya kula, kucheza ngoma, kuimba, kupiga ngoma na kadhalika na shughuli hiyo huwa ni ya siku nzima.

Lakini pia husherehekea Kwa kawaida wenyeji hupata mlo mara mbili kwa siku lakini chai ya mchaichai hunywewa muda wowote sikukuu za kidini za Kikristo hasa Krismasi na Pasaka kwa sehemu ambazo Ukristo umeingia.

Wenyeji katika vijiji vya asili wana utaratibu wao wa kuwahukumu wakosaji hasa wachawi kwani wana mahakimu wa kimila ambao wengi wao huwa ni machifu japokuwa mijini kwa siku hizi kuna mahakama za kawaida ambazo hutumia sheria za Waingereza.

Hata hivyo, mahakama za machifu ni mbaya kutokana na kuhukumu wachawi kuuawa tena kwa kuchomwa na vitu vyenye ncha kali kama vile mikuki au mishale tena basi mbele ya hadhara.

Mauaji ya aina hiyo yaliwahi kulaaniwa miaka ya hivi karibuni na mataifa mbalimbali duniani wakiwemo Wamarekani. Ambao mtoto wa makamu wa rais wan chi yao, Nelson Rockeffeler aliliwa na watu wa huko. Itaendelea wiki ijayo

 

Comments are closed.