Ndoa ya Husna Yapigwa Kalenda

Pichani ni Husna na mumewe wa awali.

MSHIRIKI wa Miss Tanzania 2012, Husna Maulid ambaye Februari, mwaka huu ilikuwa aolewe kwa mbwembwe zote na mwanaume wake raia wa Congo, Mwami Rajabu, hatimaye shughuli hiyo imesogezwa mbele.

Mwishoni mwa mwaka jana, msanii huyo alijitapa kuwa, Februari mwaka huu atakuwa mke halali wa Mwami, kwa kuwa alikuwa ameshavalishwa pete ya uchumba na vikao vya harusi vilikuwa vimeanza na mwandani wake akithibitisha hilo, ndipo ikamlazimu paparazi wetu kumvutia waya kujua kinachoendelea baada ya muda kupita.

Husna.

“Msione kimya kila kitu kiko poa, ila tu harusi tumeisogeza mbele kidogo, tunatarajia kufunga ndoa Mei 12, mwaka huu hapahapa jijini Dar,”alisema. mwaka huu ilikuwa stori.

Na Mwandishi Wetu/GPL


Loading...

Toa comment