The House of Favourite Newspapers

Malaika: Naanzaje Kuuza Mwili Marekani?

Malaika wa kwanza (kulia) akiwa na raia wa Marekani nchini humo

Na ANDREW CARLOS| GAZETI LA IJUMAA| STAR MIX

MSANII wa muziki Bongo ambaye hivi karibuni alitimkia Marekani kwa shughuli za kimuziki amegandwa na skendo ya kujiuza maeneo mbalimbali nchini humo na ikatajwa kuwa ndiyo sababu ya kuzamia huko mazima.

Habari hizo zilizagaa mtandaoni hivi karibuni, huku baadhi ya watu waliojifanya kumjua sana wakidai kuwa, wakati msanii huyo anaondoka Bongo ilikuwa akakae siku chache lakini amegoma kurudi na miongoni mwa mishe anazozifanya ni kujiuza kwenye makasino na sehemu za burudani.

Malaika (kulia) akiwa na mtanzania anayeishi Marekani.

Baada ya madai hayo kuzagaa, paparazi wetu alimtafuta Malaika kupitia simu yake kwa njia ya WhatsApp ambapo alipopatikana alisema:

“Jamani, naanzajeanzaje kujiuza? Huku nimekuja kwa dili zangu za kimuziki, hao wanaonizushia kuwa najiuza ni kati ya wasionitakia mema.”

 

Comments are closed.