Harmorapa Auza Sura na Mzungu wa Kampuni ya Swala Escape One

Athuman Omary ‘Hamorapa’.

Salum Milongo/GPL

MSANII wa Bongo Fleva anayetrendi katika mitandao ya kijamii Bongo, Athuman Omary ‘Hamorapa’, jana jumamosi katika viwanja vya Escape One Kinondoni Jijini Dar es Salaam, alionekana kumganda mzungu wa kampuni ya kinywaji cha Swala baada ya kusambaa kwa taarifa za kupewa dili nono na kampuni inayozalisha kinywaji cha Swala.

Harmorapa na Mzungu wa kampuni ya Swala.

Kupitia mtandao wake wa kijamii wa Hamorapa, imeweka Ujumbe akijinadi kwa mashabiki wake kuwa yupo na mzungu wake bosi wa kijanywaji hicho.

Aidha kwa sasa mashabiki wanamshauri Hamorapa kufanya kazi nzuri za sanaa na kuachana na kiki zisizo na kichwa wala miguu.

Toa comment